WACHEZAJI COASTAL ‘KULAMBA’ MILIONI 20 WAKIIFUNGA MTIBWA




Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, Mzee Mchemi Mohamed ameahidi kuwapa milion 20 wachezaji wa timu hiyo ikiwa tu wataifunga na kuitupa nje ya michuano ya kombe la FA timu ya Mtibwa Sugar na kutinga robo fainali.
Mchemi ambaye alikuwa kiongozi wa timu hiyo ya Tanga kwa miaka 12 (1970-1998) na kuisaidia kushinda ubingwa wa ligi kuu Bara mwaka 1988 ametoa ahadi hiyo muda mfupi baada ya wachezaji wote wa timu hiyo kupiga picha ya pamoja wakiwa na bango lenye maandishi yenye kudai mishahara yao.
Wagosi wa Kaya watawakaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa hatua ya 16 Ijumaa hii katika uwanja wa Mkwakwani. Wachezaji wanadai malimbikizo yao ya mishahara, posho kwa miezi mitatu sasa lakini wamesema wataendelea kucheza mpira kwa kuwa ni kazi yao.
“Suala la kutokucheza mpira kwa kweli hilo halipo katika akili zetu. Sisi kama wachezaji tumeangalia lile ambalo ni haki yetu ya msingi. Wanachama ndio wenye jukumu sababu Coastal ni timu ya wanachana, kwa hiyo wanachama ndiyo watafanya maamuzi yao ambayo wanaona yako sahihi juu ya uongozi wao.”
“Sisi linalotuhusu ni hela, hela ambayo tuna haki ya kuidai. Kimatokeo hatuko vizuri, nafasi yetu katika msimamo wa ligi hatuko vizuri. Hiki ni kipindi cha ukweli, hatuwezi kufanya kazi tu wakati tuna familia zinatutazama.” anasema mmoja wa wachezaji hao kwa niaba ya wachezaji wenzake.
Wanachama wa timu hiyo wamemtaka mwenyekiti wao Dr. Twaha kujiuzulu na kuendelea na kazi zake. Mwenyekiti huyo wa Coastal amekuwa akitumia muda mwingi katika shughuli zake binafsi jijini Dar es Salaam, hana ukaribu na timu, na mbaya zaidi hata timu yake ikiwa na mchezo Dar es Salaam hafuatilii chochote.
Katibu mkuu wa klabu amekuwa akijiongezea mishahara na sasa analipwa kiasi cha Tsh. milioni 1 kwa mwezi.
“Mwenendo wa timu yetu si mzuri, nawaahidi wachezaji kuwalipa mishahara yao yote kama watamfunga Mtibwa. Wanipe raha wamfunge Mtibwa nitawapa milioni 20”, anasema mzee Mchemi.



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: