JUA kali anti, panda twende,” dereva wa gari dogo aina ya Toyota Vitz alimwambia
Mage huku akipunguza mwendo na kutembea naye sambamba.. .
“Asante , nashukuru,” alijibu Mage huku
mkono wake wa kulia akiwa ameutumia
kuweka mkoba wake juu ya kichwa ili
kuziba jua lililokuwa likimchoma alasiri
hiyo.. .
“Twende dada … ”
“Nimesema asante jamani ah!” alisema
Mage, safari hii kwa ukali kidogo .
“Nisamehe anti kama nitakuwa
nimekukera. ”
“Tena sana tu, ” alisema Mage akiangalia
pembeni .
Dereva huyo aliongeza mafuta, akaondoka
zake.. .
“Mijitu mingine bwana , inaamini kuwa na
gari ndiyo njia pekee ya kumpata
mwanamke. Mwone kwanza, ” alisema
mwenyewe Mage.
Ni kweli 0 jua lilikuwa kali sana japokuwa
ilipata saa tisa alasiri . Mage alikuwa
akitembea kutoka nyumbani kwake Kimara
kwenda kituoni kupanda daladala kwenda
kwenye kikao cha harusi Kinondoni .. .
“Da ! Lakini kweli jua ni kali sana, ” alisema
moyoni, akatumbukiza mkono kwenye
mkoba na kutoa kitambaa ili kujifuta jasho
jembamba lililoanza kumchuruzika.
Hatua kama kumi na tano tangu akatae lifti
ya Vitz, Mage alipungia mkono Bajaj. ..
“Unaweza kunipeleka Kinondoni ?”
“Sawa .”
“Itakuwa shilingi ngapi ?”
“Elfu kumi tu. ”
“Eti elfu kumi tu. Yaani elfu kumi we
unaiona ndogo mpaka unasema tu? Mimi
nina elfu nane tu. ”
“Na wewe elfu nane unaiona kubwa mpaka
unasema tu? Haya twende .”
Mage alipanda akiwa anacheka majibu ya
dereva huyo wa Bajaj .. .
“Usikimbize please. ”
“Usijali dada , mimi dereva mzuri sana .”
“Ohoo! Wapo wenzako walisemaga
hivyohivyo matokeo yake wakanitumbukiza
kwenye mtaro ,” alisema Mage.
“Kwani ni mara yako ya kwanza kupanda
Bajaj anti?”
“Ndiyo usafiri wangu mkubwa kila siku
kama nina shida ya kwenda mahali .”
“Basi kumbe utakuwa umejua Bajaj ni bora
kuliko bodaboda . ..”
“Tena usinitajie hao watu wa bodaboda . ”
“Kwa nini anti ?”
“Hawajitambui . Wanachojua wao ni kusukuma mbele bodaboda lakini si kujua
wapi wapite, muda gani na mahali gani!”
***
Bajaj iliendeshwa kwa uangalifu mkubwa
mpaka Kinondoni , Mage akashuka
alikotakiwa kushuka , akalipa akaingia
kwenye baa ambayo ilikuwa na kikao.
Aliwahi kwa vile yeye ni katibu.
Wajumbe wa kikao walianza kuwasili
mmojammoja, Mage akiwa ameshafika . Kila
mjumbe alipofika yeye alimwandika jina na
kumpa karatasi yenye maelezo ya kikao
kilichotangulia. Miongoni mwa wajumbe
waliokuwa wakifika , wengine walikuwa
kwenye magari yao, wengine walishuka
kwenye Bajaj , wengine na bodaboda. ..
“Yaani hata wewe Martha unapanda
bodaboda?! Huogopi ?” Mage alimuuliza
Martha ambaye ni mjumbe wa kikao hicho.
“Niogpe nini sasa Mage? Kuna usafiri mzuri
na wa haraka kama bodaboda ?”
“Mh ! Ajali je?”
“Ajali ni bahati mbaya , mbona hata malori
yanapata ajali, sembuse bodaboda!”
“Da ! Mi sijawahi na sitaki kujaribu .
Nitaendelea kupanda Bajaj mpaka basi.”
Kikao cha harusi kilianza baada ya
mwenyekiti wake kufika na wajumbe
kukidhi akidi !
Kikao kilienda vizuri huku wajumbe,
akiwemo Mage wakiruhusiwa kupiga ulabu
watakavyo kutokana na fedha za uchakavu
wa wiki iliyopita .
Kidogokidogo wajumbe walianza kulewa ,
hata mazungumzo yao yaliashiria hivyo. ..
“Sasa jamani nadhani tuje kwenye
kipengele cha ahadi, kama kuna mtu
anataka kutoa ahadi aseme , kama kuna
mtu alishaahidi anataka kupunguza afanye
hivyo, harusi yetu sote jamani ,” alisema
mwenyekiti huku glasi yenye bia ikiwa
mkononi tayari kwa kuipeleka kinywani.. .
“Mimi wiki iliyopita nilisema nitatoa
shilingi laki moja lakini leo naongeza na
gari la kubebea wazazi wa bwana harusi ,”
alisema mjumbe mmoja anaitwa Zakayo
huku akinesanesa kwa ulevi. ..
“Paa paa paa,” wajumbe walipiga makofi .. .
Baadhi ya wajumbe walishangaa kwani
wanavyomjua Zakayo hana hata baiskeli
sasa kusema atatoa usafiri kwa wazazi wa
bwana harusi kwao ilikuwa ni mshangao .. .
“Labda atawakodishia,” alisema moyoni
mwanamke mmoja aitwaye mama Maende
ambaye ni jirani na Zakayo.. .
“Mimi nitatoa usafiri kwa maharusi,
kutokea kanisani hadi ukumbini na kutoka
ukumbini kuwapeleka fungate ,” alisema
mzee Majaribio huku sauti ikianza kutoka
kwa kukawaruza kutokana na ulevi wa
kuanza mapema . Huyu mzee Majaribio
anamiliki magari mawili lakini mtaani
anasifika kwa uchoyo wa lifti. Yeye hata
kama kuna mvua, akimwona jirani
anatembea kwa miguu anageuzia macho
pembeni au kama atasimamishwa kwa
kuitwa kwa sauti , atauliza. ..
“Unaelekea wapi wewe ?”
“Mimi kanishushe pale Rombo.. .”
“Aaah ! Napita chuo , pole sana .”
Hata kama hapiti chuo .
Baadhi ya wajumbe wanaomfahamu
walimshukuru Mungu kuona kama kweli
mzee Majaribio ataweza kutoa gari lake
kwa ajili ya maharusi . Na gari alilojua ni
moja kwani ndiyo jipya .
Saa mbili usiku, kikao kilimalizika, sasa
ikawa maongezi ya wajumbe na bia juu .
Mwenye kucheka alicheka, mwenye kulalia
kiti sawa , Mage alikuwa akisinzia huku
simu zake mbili zipo mezani.
Saa tano usiku ilifika kama mchezo ,
wajumbe walianza kuchomoka
mmojammoja bila kuaga .
Mage naye alijikokota hadi kituo cha
daladala kutafuta usafiri wa Bajaj .. .
“Anti twende,” dereva wa bodaboda
alimwambia
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment