WAPENZI wa Soka la England watakuwa na burudani murua Wikiendi hii wakati Ligi Kuu England, BPL, ikiwa dimbani baada ya Wikiendi iliyopita kupisha FA CUP na pia Jumapili ipo Fainali ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, C1C.
BPL itaanza mapema Jumamosi kwa Mechi kati ya West Ham na Sunderland na kufuatiwa na Mechi kadhaa ikiwemo ile ya Vinara wake Leicester City kucheza Nyumbani na Norwich wakati Mabingwa Watetezi Chelsea wakiwa Ugenini kuivaa Southampton.
BPL itamaliza Jumamosi kwa Mechi kati ya West Bromwich Albion na Crystal Palace.
Jumapili ndio hasa Siku ya Bigi Mechi ambapo ipo Fainali ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, C1C, kati ya Liverpool na Man City Uwanjani Wembley Jijini London.
Lakini kabla ya Fainali hiyo kuanza mambo yote yapo Old Trafford ambako Man United watachuana na Arsenal kwenye Mechi ya BPL.
+++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP-FAINALI
-Wembley Stadium, London
Jumapili Februari 28
**Saa za Bongo
1930 Liverpool v Man City
+++++++++++++++++++++++
Bila ya Timu kupata mapumziko ya kutosha, Timu zote 20 za BPL zitatinga tena Viwanjani kucheza Mechi za Ligi na Bigi Mechi katika duru hili ni Jumatano huko Anfield wakati Liverpool wakicheza tena na Man City ndani ya Siku 3.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumamosi Februari 27
1545 West Ham v Sunderland
[Mechi zote kuanza 1800]
Leicester v Norwich
Southampton v Chelsea
Stoke v Aston Villa
Watford v Bournemouth
2030 West Brom v Crystal Palace
Jumapili Februari 28
[Mechi zote kuanza 1705]
Man United v Arsenal
Tottenham v Swansea
Jumanne Machi 1
[Mechi zote kuanza 2245]
Aston Villa v Everton
Bournemouth v Southampton
Leicester v West Brom
Norwich v Chelsea
Sunderland v Crystal Palace
Jumatano Machi 2
2245 Arsenal v Swansea
2245 Stoke v Newcastle
2245 West Ham v Tottenham
2300 Liverpool v Man City
2300 Man United v Watford
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment