Hatma ya LOUIS VAN GAAL kuendelea kuifundisha Manchester United angalau mpaka mwishoni mwa msimu inazidi kupata wakati mgumu – LVG atakuwa na siku 11 mwezi ujao ambazo zinaweza kuamua hatma yake ndani ya Old Trafford.
Mechi hizi kwa kiasi kikubwa zitatoa picha kamili ya msimu wa United utaishaje – je mbio za nafasi 4 kwenye EPL zitakuwaje, Wataweza kufika nusu fainali ya FA Cup kwa kuitoa West Ham na hatma yao kwenye michuano ya ulaya ipo mikononi mwa Liverpool.
Miaka miwili iliyopita David Moyes alifukuzwa baada ya Red Devils kuthibitishwa kimahesabu kwamba hawatoweza kushiriki kwenye michuano ya ulaya na LVG anaweza kukutana na kilichomkuta mwenzie ikiwa atashindwa kupata matokeo katika mechi hizo muhimu.
Jose Mourinho anatarajiwa kuchukua mikoba ya boss wake wa zamani mwishoni mwa msimu hata hivyo, ingawa matokeo mazuri kwa LVG yanaweza kuendelea kuifanya bodi ya klabu hiyo kuendelea kugawanyika juu ya kuchukua maamuzi dhidi yake – lakini ikiwa atafeli katika mechi hizo muhimu basi bodi itakuwa haina namna zaidi ya kuchukua maamuzi magumu juu yake.
Ikiwa kocha huyo mdachi akafanikiwa kubadilisha upepo na kubeba vikombe vya FA na Europa – basi anaweza kuendelea msimu ujao na kufanikiwa kumaliza mkataba wake wa miaka 3
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment