[Story]: KITANDANI KWA BABA MWENYE NYUMBA......sehemu ya 10 chombezo




ILIPOISHIA  ..

“Mpenzi, chumba kimepatikana…”
“Wapi..?”
“Kule maeneo ya nanihi, si mbali
sana…”
“Bonge la chumba. Simenti chumba
chote, kikubwa kama uwanja wa mpira, halafu bei ya ubwete…”

“Ngoja kwanza, una maana mimi
nitaweza kuja na gari nikaegesha mahali..?”
“Mh! mh! Mwenye nyumba anaweza
kutengeneza pakingi ana nafasi kubwa…”

***
Baba Joy alikuwa amekaa kwenye
mgahawa mmoja mpya. Hauna watu wengi na uko mtaa wa pili kutoka nyumbani kwake.
Simu yake iliisha chaji na alikuwa akipigania kuchajiwa na mwenye mgahawa huo…
“Chaja ya pini ndigo ilikuwepo mzee,
sijui nani kaichukua? We Benadi…” Benadi ni mhudumu wa mgahawa huo…
“Nani kachukua chaja ya pini
ndogo..?”
“Sifahamu bosi, muulize Malinda jana
alikuwa analalamika simu yake haina chaji,” alijibu Benadi.
Baba Joy alitoka mbio hadi nyumba ya
pili baada ya mgahawa huo. Nyumba ambayo hakuna anayemjua…
“Jamani hodi…”
“Karibu,” binti mmoja, mweupe, mnene
kiasi alitoka na kumwangalia kwa tabasamu mzee huyo…
“Karibu sana…”
“Asante…”
“Shikamoo…”

“Marhaba, shida yangu chaja, nipo
kwenye mgahawa huo na kuna mtu wa muhimu sana natakiwa kumpigia, simu imeisha
chaji.”
Yule binti alinyoosha mkono ili
aipokee simu hiyo huku akisema…
“Au ulitaka chaja ukachajie hapo
mgahawani..?”

“Ndiyo maana yangu, itakuwa si mbaya
sana,” baba Joy alisema huku akionesha dalili za kuchanganyikiwa. Alimini kuwa,
endapo ataiacha simu yake pale ndani akipigiwa na Helena au Fuko hatajua.
Yule binti aligeuka kurudi ndani
akimaanisha anakwenda kuchukua chaja. Baada ya muda alirejea…
“Hii, si utairudisha mwenyewe..?”
“Usajali binti, nitairudisha mimi
mwenyewe, nakushukuru sana binti yangu…”
“Usijali baba.”

Baba Joy alitoka haraka na chaja hiyo
hadi kwenye ule mgahawa…
“Ee bwana nimebahatisha chaja, naomba
nichomekee kwenye soketi yenu basi.”
Chaja ilipokelewa, ikapelekwa kwenye
soketi huku baba Joy akiwa amerudi kwenye kiti alichokaa na kuendelea  kunywa soda yake.

***
Mama Joy na mzoa taka waliongea mengi
kuhusu chumba cha kijana huyo, alimuahidi kumnunulia godoro, kitanda, kabati la
ngu, meza, redio, tivii na kapeti kubwa chini…
“Lakini nakuonya, usije ukakifanya
chumba cha kuingiza malaya wako…”
“Haitawezekana mupenzi, mimi
nakupenda wewe, kama hivi unaniwezesha, unanitengenezea maisha…”
“Hapo umesema, mimi sitaki kabisa
mwanamuem malayamalaya.”

Mama Joy aliposema hataki wanaume
malayamalaya, mzoa taka alitamani kusema…
“Mbona we malaya tu.”

Mama Joy akijua muda unakwenda,
alianza kwa kumshikashika mzoa taka sehemu mbalimbali za mwili…
“Sasa kijana ukiwa unajua tutakutana
uwage unaoga hata kidogo jamani…”
“Leo dawasa walizuia maji…”
“Uwe unajitahidi kuhifadhi, sawa?”
“Sawa mupenzi…”

“Halafu mi sitaki uwe unaniita
mupenzi, we ita mpenzi tu nitakuelewa,” alisema mama Joy huku akiendelea
kumshikashika kijana huyo, mwili ulimsisimka, damu zilimtembea kwa kasi,
akaanza kuhisi kuzimiazimia kwa raha na yeye akapeleka mkono kwenye ‘nido’ la
kulia la mwanamke huyo, mama Joy akaruka kidogo...
“Wao, umejuaje kijana wangu. Hapo
uliposhika ndipo penye transifoma,” alisema mama Joy.

***
Helena aliamua kuweka wazi kwa Fuko
akiamini hata yeye amekatiwa kitu kidogo chake…
“Mimi alinipa hela, lakini hapa hoja si
hela bali ni kumpata bosi ili tumwambie mzoa taka yumo chumbani mwako, tena
kitandani,” alisema Helena…
“Ni kweli, ana simu mbili, lakini ile
simu moja sijui inatumia namba gani?” alisema mlinzi. Walipiga plani ya kwenda
kwa mama Joy ili wakaombe namba lakini wakaona haiwezekani…
“Atakuuliza unataka namba yake hii ya
nini? Halafu tena mfano akikupa halafu mumewe akarudi sasa hivi na kumfumania
si atajua ni sisi kwa sababu tuliomba namba…”
“Ni kweli, itakuwa ngumu, sasa
tufanyeje?”

“Mh! tuendelee kumpigia, itakuwa simu
imeisha chaji, akiwasha tu tutampata tutamwambia…”
“Au tumtumie meseji, wewe mtumie na
mimi ili akifungua simu na kukutana nazo atajua kumbe tulimtafuta wote.”

***
Kule kwenye mgahawa, mara muuza
mgahawa alitokea akiwa ameshika ile chaja aliyokwenda nayo baba Jy pale…
“Bwana vipi, tayari mara hii?” baba
Joy aliuliza akiwa na uso wa shauku…
“Mzee hii chaja kumbe ni ya pini
kubwa, sijui itakuwaje?”
“Haa!” baba Joy alihamaki, picha ya
mzoa taka na mkewe mama Joy ilimwingia hivihivi anaona kwa sababu tu ya kukosa
mawasiliano…
“Ile simu ingekuwa nzima ningeitumia,
sasa…”

***
Kule chumbani, mama Joy na mzoa taka
mchakato ulikolea kupita kawaida. Mapenzi yalikuwa motomoto, kila sehemu ya
kitanda ilitoa mlio wa masikitiko kwa kulemewa na uzito wa walio juu.
Mzoa taka alijituma kuliko jana na
juzi. Mama Joy alikuwa mtu wa ‘kulalamika’ tu kama yuko na mumewe. Hakujali
kwamba baba Joy angeweza kurejea nyumbani hapo ghafla na kuwanasa.
Mlinzi, baada ya kumkosa baba Joy
kwenye simu alifanya doria. Alikuwa akienda ndani na kusimama kwenye mlanngo wa
mama Joy kisha kurudi getini. Kuna wakati alipokuwa amesimama hapo mlangoni,
Helena naye alitokea…
“Bado wapo?”
“Bado, tena bosi anapiga kelele sana,
huyu mwanamke anatafuta matatizo,” alisema mlinzi.

***

“Basi jamani nawaombeni nipe simu
yenu mi niweke laini yangu mara moja, kuna mtu nataka kuwasiliana naye dakika
moja tu,” baba Joy alimwambia yule mwenye mgahawa ambaye naye alitoa laini na
kumpatia simu yake.

Baba Joy aliweka laini kwenye simu
hiyo na palepale meseji zikaanza kumiminika kwa wingi.
Mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi
huku akiwa kama anazisoma meseji hizo kwa hisia kabla ya kuzifungua…
“Bosi hupatikani kwenye simu,
umezima. Mzoa taka ndani ya nyumba hapa.” Hiyo ilikuwa meseji kutoka kwa
Helena…
“Bosi, mwizi wako keshaingia sasa,
kazi kwako ukichelewa utamaliziwa uhondo wote ohooo.” Huyo alikuwa mlinzi.
Baba Joy hakutaka kupoteza muda kwa
kusoma meseji nyingine, alimpigia Helena…
“Bosi yumo bado yumo chumbani,”
alisema Helena.

Baba Joy alikata simu. Kwa machungu
na maumivu ya wivu alijikuta akitaka kuondoka na simu ya watu…
“Sasa mzee wangu mbona unaondoka na
simu halafu hii chaja vipi, umeazimia wapi? Soda pia hujalipa mzee wangu.”
“Ooo, sorry. Chaja ya nyumba ya pili
hapo, simu yako hii, samahani kwa kutolipa,” alisema baba Joy huku akitoa noti
ya shilingi elfu kumi ambayo hakusubiria chenji.

Aliingia ndani ya gari lake na
kuondoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwake. Barabarani nusura agonge magari
mengine. Akili yake ilikuwa haimwambii nini cha kufanya baada ya kufika huko…
“Hivi nikiwakuta laivu niwafanyaje?
Niwaue wote, nimuuze yule mshenzi, niwatoa nje na kuwatembeza uchi au? Nitajua
hukohuko,” alisema moyoni baba Joy. Hapo alikuwa akikata kona kuingia barabara
inayoelekea kwake.

Alipofika getini hakutaka kupiga
honi. Aliegesha gari na kushuka akiacha mlango wazi.
Bahati njema kwake alikuta geti liko
wazi, akazama ndani na kumwona mlinzi akitokea ndani…
“Bosi wapo chumbani,” mlinzi
alimwambia kwa sauti ndogo. Baba Joy alisimama kwanza na kukumbuka bastola
ameiacha kwenye gari. Alirudi mbio, akaichukua na kwenda ndani. Alitembea kwa
mwendo wa kunyata wakati anaukaribia mlango wa chumbani.
Ulikuwa wakati mgumu sana kwake,

stori by IRENE MWAMFUPE
*USIKOSE SEHEMU YA 11..HAPA*


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: