STAA MPYA OLD TRAFFORD, MARCUS RASHFORD, AVUNJA REKODI YA MIAKA 51 YA GEORGE BEST!


MANUNITED-MARCUS-RASHFORD-BESTMARCUS RASHFORD, akiwa na Miaka 18 na Siku 117, ameweka Historia katika Klabu ya Manchester United ya kuwa Mfungaji mwenye Umri mdogo kwa Mechi za Ulaya wakati alipopiga Bao 2 Man United walipoitwanga FC Midtjylland 5-1 Jana Usiku.
Rekodi ya Mfungaji mwenye Umri mdogo iliwekwa na George Best Oktoba 1964 wakati Man United inaitwanga Djurgarden Bao 6-1 katika Mashindano ya Ulaya yaliyokuwa yakiitwa Inter-Cities Fairs Cup.
Wakati huo George Best alikuwa na Umri wa Miaka 18 na Siku 158.
Alhamisi Usiku, Marcus Rashford, aliecheza Mechi kibahati tu baada ya Anthony Martial kupata maumivu wakati akipasha moto mwili kabla Mechi kuanza, alifunga Bao 2 na kuivunja Rekodi ya George Best ya Miaka 51 na vile vile kuipaisha Man United kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
HABARI ZA AWALI:
EUROPA LIGI: KINDA MIAKA 18, SHUJAA MPYA MAN UNITED IKISHINDILIA 5!
BILA kutegemewa Kijana wa Miaka 18, Marcus Rashford, aliekuwa kapangwa Benchi alilazimika kuanza Mechi hii na hakutetereka kwa kuifungia Manchester United Bao 2 walipoishindilia FC Midtjylland Bao 5-1 na kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI kwa Jumla ya Bao 6-3 baada ya kupoteza Mechi ya kwanza 2-1.
Kabla ya Mechi kuanza Man United walipata pigo kubwa baada ya Anthony Martial, ambae alipangwa kuanza Mechi hii, kuumia wakati akipasha moto na nafasi yake kuchukuliwa na Chipukizi Marcus Rashford ikiwa Mechi yake ya kwanza kabisa kuchezea Timu ya Kwanza.
Pigo hilo lilifanya Benchi la Man United kubakia na Wachezaji wa Akiba 6 tu kwenye Benchi badala ya wale 7 wanaotakiwa kuwepo.
FC Midtjylland walitangulia kufunga Dakika ya 28 kwa Bao la Pione Sisto lakini Dakika 4 baadae Bodurov alijifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa Krosi ya Memphis.
Dakika ya 42 Man United walipewa Penati kutokana na Andre Romer kumuangusha Herrera lakini Juan Mata alipiga mkwaju wa Penati hiyo kidhaifu na Kipa Andersen kuokoa.
Hadi Mapumziko Man United 1 FC Midtjylland 1.
Dakika ya 64 pasi ya Juan Mata ilimkuta Marcus Rashford aliefunga na kuwapa Man United uongozi wa Bao 2-1.
Dakika ya 75, si mwingine tena bali Kijana mpya wa Kitaa, Marcus Rashford, aliepiga Bao la 3 kwa kuunganisha Krosi ya Varela.
Herrera aliipa Man United Bao la 4 kwa Penati katika Dakika ya 88 na Memphis kushindilia Bao la 5 Dakika ya 90.
Man United sasa wamesonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na watamjua mpinzani wao Kesho Alhamisi Februari 27 baada ya Droo itakayofanyika huko Nyon, Uswisi.
VIKOSI:
Manchester United: Romero; Varela, Carrick, Blind, Riley; Schneiderlin, Herrera; Lingard, Mata, Memphis; Marcus Rashford
Akiba: J. Pereira, Rojo, Poole, McNair, Love, A. Pereira
FC Midtjylland: Andersen, Romer, Hansen, Bodurov, Novak, Sparv, Poulsen, Olsson, Hassan, Sisto, Urena
Akiba: Pusic, Kadlec, Dahlin, Banggaard Jensen, Bak Nielsen, Onuachu, Royer
REFA: Istvan Vad (Hungary)
Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Matokeo:
Jumatano Februari 24
Sporting Braga 2 Sion 2 [Bao 4-3 kwa Mechi mbili]
Alhamisi Februari 25
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2
Lokomotiv Moscow 1 Fenerbahce 1 [1-3]
Athletic Bilbao 1 Marseille 1 [2-1]
Rapid Vienna 0 Valencia 4 [0-10]
Liverpool 1 Augsburg 1 [0-0]
Krasnodar 0 Sparta Prague 3 [0-4]
Lazio 3 Galatasaray 1 [4-2]
Schalke 0 Shakhtar Donetsk 3 [0-3]
Bayer Leverkusen 3 Sporting Lisbon 1 [4-1]
Molde 1 Sevilla 0 [1-3]
Napoli 1 Villarreal 1 [1-2]
Porto 0 Borussia Dortmund 1 [0-3]
Olympiacos 1 Anderlecht 0==Dakika 90 [Baada ya Dakika 120, 1-2 Mechi mbili 1-3]
Tottenham 3 Fiorentina 0 [4-1]
Basle v St Etienne [2-3]
Manchester United 5 FC Midtjylland 1 [6-3]
KALENDA
Raundi ya Timu 16-Droo: 26 Februari, Nyon
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswis



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: