MKUDE AOMBA MSHIKAMANO SIMBA SC, ASEMA LIGI BADO HAINA MWENYEWE


ALIYEKUWA Nahodha wa Simba SC katika mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga SC mwishoni mwa wiki, Jonas Gerald Mkude ameomba wanachama na wapenzi waendelee kuisapoti timu ili itimize malengo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE baada ya kupoteza mchezo wa watani kwa kufungwa 2-0 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mkude amesema kwamba wamesikitishwa mno na matokeo hayo, lakini wanapswa kusimama imara na kusonga mbele.
Jonas Mkude ameomba mshikamano Simba SC 

“Kama ilivyo kaulimbiu yetu Simba, Nguvu Moja, sasa tutawekeza nguvu zetu kwenye michezo inayofuata na ni matumaini yetu bado wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba tutakuwa pamoja katika kuendelea kuhakikisha kuwa ubingwa msimu huu unakuja Msimbazi,” amesema.
Simba SC ilipokonywa usukani wa Ligi Kuu baada ya kuchapwa 2-0 watani wao, Yanga mabao ya Mzimbabwe Donald Ngoma kipindi cha kwanza na Mrundi Amissi Tambwe kipindi cha pili.
Matokeo yaliifanya Yanga ifikishe pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda kileleni, wakati Simba SC iliyocheza mechi 20, inaporomoka hadi nafasi ya tatu ikibaki na pointi zake 45, sawa na Azam FC nayopanda nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao (GD).


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: