Kuelekea Arsenal vs Barca; MSN wana rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi kuanzia hatua mtoano


Msimu wa 2015-16 wa Champions League umefikia hatua ngumu za mtoano – na hatua hizi ndio ambapo wale vijana watatu wa Amerika ya kusini, Neymar, Messi na Suarez wamekuwa wakifunga sana.
  Msimu wa 2014/15 FC Barcelona walifanikiwa kufunga magoli 16 katika michezo ya mtoano – na magoli 14 kati ya hayo 16 yalifungwa na MSN. Ni Ivan Rakitic, ambaye alifunga goli katika hatua ya 16 bora dhidi ya Manchester City na lingine akafunga kwene fainali. 
  Neymar alifunga magoli 7, Suarez akapiga 5 na Messi akafanikiwa kufunga mawili – na pia alihusika sana katika kutengeneza magoli. Katika hatua ya makundi wachezaji wengi walihusika na ufungaji. Suarez alifunga matano, Rakitic na Neymar walifunga mawili mawili,  Pique, Adriano na Sergi Roberto wote walifanikiwa kufunga goli moja moja – jumla ya magoli yote ni 15 katika hatua ya makundi. 
  Msimu huu wa 2015/16 – FC Barcelona wamefunga tena magoli 15 katika hatua ya makundi – na leo usiku wanaingia kwenye mchezo dhidi ya Arsenal katika hatua ya mtoano – Je wataanza mechi ya leo kwa kufunga magoli mangapi



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: