Lionel Messi alikuwa na miaka tisa tu kwao Argentina wakati Kocha Arsene Wenger alipojiunga na Arsenal mwaka 1996.
Wenger alijiunga na Arsenal akitokea Grampus Eight ya Japan na kuchukua nafasi ya Graham Taylor.
Leo Arsenal inakutana na Barcelona ikiwa mwenyeji katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 Bora.
Presha kubwa ya Wenger ni kwa kijana Lionel Messi ambaye alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13.
Messi alisafiri akitokea kwao Rosario, Argentina na kuungana na Barcelona akiwa na baba yake mzazi aliyelazimika kuacha kazi ili kumsaidia mwanaye aliyekuwa akiugua ugonjwa wa kushindwa kukua kwa mwendo sahihi.
Wenger ana misimu 19 na Arsenal, lakini hiyo haimalizi hofu ya Mfaransa huyo dhidi ya kijana machachari kabisa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment