TAMBWE AMUWASHIA INDIKETA KIIZA, AMWAMBIA AKAE PEMBENI


STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe na Hamisi Kiiza wa Simba wapo kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kiatu cha Dhahabu lakini Tambwe amemwambia Kiiza akae pembeni kwani hawezi kutwaa kiatu hicho japokuwa amemzidi goli moja.


Mpaka sasa Kiiza amefikisha mabao 16 huku Tambwe akiwa na mabao 15 na amejipa matumaini makubwa ya kutwaa kiatu hicho ambacho amewahi kukibeba wakati huo anaichezea Simba alipofika mabao 17.

Akizungumza na njenje habari, Tambwe alisema kuwa "Nitaendelea kupachika mabao kwasababu napata ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzangu pamoja na viongozi wangu hivyo huyo Kiiza awe tayari kutoka kileleni

"Simba waliniacha kwa madai kuwa kiwango changu kimeshuka ila nawadhihirishia kuwa nipo vizuri na ninashukuru nathibitisha hilo hata kwenye mechi tunazokutana nao, wanajisifu wana safu nzuri ya ulinzi na hawajafungwa mechi sita ila sisi tumewafunga, nikiamua jambo hakuna anayeweza kunizuia, kama
nilivyoamua kuwafunga wao katika mechi hiyo ya juzi," alisema Tambwe


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: