Mchungaji wa kanisa la Evangelist
Assemblies of God Tanzania (EAGT) katika kijiji cha Mgongoro kata ya
Igunga mkoani Tabora, Abel Godfrey, amekamatwa na waumini wake baada ya
kudaiwa kukutwa akifanya mapenzi na binti wa kaka yake.
Waumini hao wakishirikiana na
uongozi wa serikali ya kijiji hicho, walifanya tukio hilo juzi saa 5:30
usiku akiwa na binti huyo umri wa miaka 20 jina tunalihifadhi mwenye
mtoto mchanga wa miezi minne.
Akizungumza kwa masikitiko babu wa
binti huyo, Bictoni Kyarero, alisema mchungaji Godfrey, alikuwa na tabia
hiyo kwa mwaka mmoja sasa, lakini tabia hiyo ilimchosha na kutoa
taarifa kwa waumini wake pamoja na uongozi wa mtaa kisha kumuwekea mtego
uliomnasa akiwa katika nyumba hiyo.
Amesema baada ya kumkamata alijaribu
kukimbia lakini walifanikiwa kumdhibiti na kisha kukiri kufanya mapenzi
na binti huyo huku akiwabembeleza waumini wake wamfichie siri.
Kwa upande wake binti huyo
alipoulizwa kuhusu kufanya uzinzi na baba yake mdogo, alikiri huku
akisema alitenda kosa hilo baada ya kutishwa na mchungaji huyo iwapo
angekataa angemuombea kwa Mungu ili awe kichaa.
Akizungumzia tukio hilo, mchungaji
huyo amekiri kutenda kosa hilo na kubainisha alifanya hivyo baada ya
kuzidiwa ‘ujanja’ na shetani huku akitubu na kudai hatorudia tena kosa
hilo.
Naye mtendaji wa kijiji hicho,
Edward Kitenya, alisema mchungaji huyo walimkamata akiwa katika nyumba
ya tembe wakiwa wamelala baada ya kutandika turubai chini wakiendelea
kufanya mapenzi na binti huyo kisha kumweka chini ya ulinzi mpaka
asubuhi na kupigishwa faini ya Sh. 20,000 na kuachiwa huru.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi
waliuomba uongozi wa kanisa hilo kumvua uongozi kwa kuwa amekiuka
maadili ya uongozi na kufanya waumini kutomwamini tena kama kiongozi wa
kiroho.
Mtendaji wa kata ya Igunga, Fredrick
Masesa, amewaomba viongozi wa dini pamoja na wananchi kwa ujumla
kuzingatia maandiko matakatifu ya mwenyezi Mungu ya kutofanya vitendo
viovu ili wamtumikie kiusahihi.
Kwa upande wake mchungaji wa kanisa
la kijiji cha Mwanzugi, Fanuel Daniel, alithibitisha kukamatwa kwa
mchungaji wa kanisa la kijiji cha Mgongoro, Godfrey na kusema tayari
wamemsimamisha kutoa huduma mchungaji huyo kwa muda usiojulikana mpaka
uongozi utakapokutana wote kwa ujumla na kuongeza kuanzia sasa kanisa
hilo la Mgongoro litaongozwa na Philipo Makeremo ambaye pia ni katibu wa
kanisa
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment