JAMII
moja katika kijiji cha Manik Bazar ilimlazimisha mtoto wa kiume mwenye
umri wa miaka saba aoe mbwa, kwa imani kuwa hatua hiyo itamwondolea pepo
mbaya.
Ripoti za habari zilisema wazazi wake na wazee waliamini nyota zilitabiri mke wake wa kwanza atafariki akiwa na umri mdogo.
Hivyo basi, waliamua mke wake wa kwanza awe mbwa ndipo kusiwe na hasara akifariki.
Picha
zilizochapishwa kwenye mitandao ya habari zilionyesha sherehe ndogo ya
harusi ambapo mvulana huyo alifunganishwa ndoa na mwana mbwa aliyevishwa
mavazi ya harusi.
Baada ya sherehe kukamilika, ilisemekana mbwa huyo koko alifukuzwa kijijini na kurudishwa mitaani alikokuwa ameokotwa.
NEW YORK, Marekani
MWANAMUME
alimlazimisha mpenzi wake kutembea uchi katika barabara za jiji hili
baada ya kumpata akitumia waume wengine jumbe za kimapenzi kupitia kwa
simu ya mkononi.
Video
ilisambazwa mitandaoni ikimwonyesha mwanamke huyo akitembea akiwa
amejifunga taulo, kisha mwanamume huyo akaivuruta kwa lazima na kusikika
akisema: “Lazima tuone aibu yako. Msichana mrembo kama wewe... Utakuaje
na waume saba! Sasa kila mtu anaweza kuona.”
Mashirika
ya habari yaliripoti kuwa mwanamume huyo alimkuta mpenzi wake akituma
jumbe hizo kwa wanaume wengine na hata kuwatumia picha zake akiwa uchi,
ingawa madai hayo hayangeweza kuthibitishwa.
Mtu
mmoja alitoa maoni yake kuhusu video hiyo na kusema, “Sijui alichofanya
na wala sijali. Hakuna mtu anastahili kuaibishwa na baradhuli kama
huyo.”
CALIFORNIA, Marekani
MWANAMKE
aliamua kuachia paka wake 1,000 nyumba yake yenye vyumba vitano vya
kulala na akahamia kijumba kidogo kinachoweza kuvurutwa na trela.
Kulingana
na mashirika ya habari, Lynea Lattanzio mwenye umri wa miaka 67,
amewaacha paka wake wawe huru kufanya wanachotaka katika jumba hilo
lenye ukubwa wa futi 4,200 kwa mraba.
Iliripotiwa alianza kufuga paka katika mwaka wa 1992 na kufikia mwisho wa mwaka huo akawa na paka 96.
Mashirika
ya habari yalimnukuu akisema: “Wakati huo nilikuwa sijaolewa na sikuwa
na watoto. Nilinunua jumba hili na kushangaa kwa nini nilichukua hatua
hiyo. Sikukusudia kuwa na paka zaidi ya 1,000 lakini ilitokea tu.”
LANCASHIRE, Uingereza
POLISI
walibaki mdomo wazi wakati mshukiwa waliyemkamata alipochukua mfuko
wenye dawa ya kulevya ya heroin kutoka kwa meza yao na kuutafuna.
Ilisemekana
kuwa Alan Timperley mwenye umri wa miaka 38 alikuwa akihojiwa katika
kituo cha polisi cha Lancashire wakati alipopatikana na mfuko mdogo
wenye dawa hiyo haramu.
Afisa
wa polisi aliweka mfuko huo mezani huku akimhoji lakini ghafla,
Timperley aliunyakua na kuutafuna. Inaaminika nia yake ilikuwa kuharibu
ushahidi.
Alipofikishwa
mahakamani, alihukumiwa kifungo cha miezi minne gerezani baada ya
kukiri mashtaka ya kuhujumu utendaji wa haki pamoja na mashtaka mengine
ya awali kuhusu wizi na uporaji.
Zimekusanywa na VALENTINE OBARA
Ludewa yetu na maendeleo yetu