MOURINHO AIANDIKIA BARUA BODI YA MAN UNITED





Mo 7
Gazeti la Independent la nchini England Jumapili hii limeripoti kuwa kocha Jose Mourinho ameiandikia barua bodi ya klabu ya Manchester United kuelezea mipango yake na jinsi atakavyofanya kama atapata nafasi ya kuwa kocha wa Manchester United.
Taarifa ya gazeti hilo la Independent imesema kuwa kocha huyo ameandika barua yenye kurasa sita akiainisha mipango na mbinu atakazo zitumia kukidhi matakwa na matarajio ya klabu ya Manchester United, ikiwa ni sambamba na kukijenga upya kikosi hicho.
Mourinho ambaye alifukuzwa kazi kukinoa kikosi cha Chelsea mwezi December mwaka jana kutokana na kuanza vibaya licha ya kutwaa ubingwa msimu uliopita amekua akiota kupewa kazi hiyo tangu 2013 alipostaafu Sir Alex Ferguson, lakini United wakampa kazi hiyo David Moyes kabla ya kumpa Louis Van Gaal msimu uliopita.
Presha imezidi kupanda kwa kocha wa sasa wa Manchester United Louis Van Gaal mara baada ya jana kuzomewa na mashabiki wa timu yake Old Trafford, kufatia kupoteza mchezo wa ligi kuu kwa bao 1-0 toka kwa Southampton, goli lililofungwa na Charlie Austin, huku Van Gaal akikiri imani ya mashabiki kupotea.



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: