SHABIKI
mmoja sugu wa Arsenal, ameitikisa mitandao ya kijamii hasa kule
Uingereza baada ya kufunga ndoa na mchumba wake akiwa amevalia sare
rasmi za kuchezea za timu hiyo badala ya suti kama ilivyo desturi kwa
Bwana Harusi.
Chini
ya hashtag #Full Kit Wears# shabiki huyo anayejitambulisha kwa jina
Bizzo Musicmad alipokea jumbe za kutosha za kumpongeza kutoka kwa
mashabiki wenzake kote duniani baada ya kuchapisha picha yake ya harusi
huku akimshukuru mke wake kwa kumkubalia afunge naye ndoa akiwa amevalia
jezi nyekundu yenye nembo ya Fly Emirates, jezi nyeupe, soksi nyeupe
vilevile na daluga, ambayo ndio sare rasmi wanayovalia wachezaji wa
Arsenal kwenye mechi zao za nyumbani.
“Mke
wangu kweli ni mzuri sana aisee, katoka kazini na kunikubalia tuoane
nikiwa nimevalia sare nzima ya Arsenal bila kuwepo na matatizo,” Bizzo
aliandika.
Kituko
hicho kiligusa sana kiungo fundi wa Arsenal, Mesut Ozil ambaye kando na
kumpongeza, alimwalika wakutane naye kwenye mechi ijayo watakapovaana
na Chelsea
Ludewa yetu na maendeleo yetu