WANACHAMA
wa kikundi cha kuweka na kukopa cha Mwijangasyege kilichopo katika
Kijiji cha Isange Kata ya Isange katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
mkoani Mbeya, wameingia katika hali ya taharuki baada ya kuku wa ajabu
kukwapua fedha kiasi cha sh.430,000 na kutokomea nazo.
Tukio
hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wanakikundi hao
walikuwa katika eneo lao la kukutania wakihesabu fedha hizo kwa lengo la
kugawana ndipo kuku huyo alipojitokeza akudonoa pesa hizo na kukimbia
kusikojulikana.
Kwa
mujibu wa maelezo ya wanakikundi hao, fedha zilizochukuliwa na kuku
huyo ambaye wao walidai kuwa ametumwa kishirikina zilikuwa shilingi
430,000 ambazo zilikuwa zimeshahesabiwa zikatengwa pembeni.
Hamu
Kitaje, ni miongoni mwa mwawanakikundi hicho ambapo alisema kuwa kuku
huyo alikwapua pesa hizo kwa kasi kubwa mithiri ya mwewe anapokwapua
vifaranga vya kuku na kwa kasi hiyohiyo aliyoingia nayo akapotea.
Alidai
kuwa mpaka sasa wanashindwa kuelewa kilichokuwa nyuma ya kuku huyo kwa
kuwa siotukio la kawaida, na moja kwa moja akalihusisha tukio hilo na
mambo ya ushirikina akidai kuwa kwa vyovyote vile alikuwa ametumwa na
mtu.
Kitaje
alisema kuwa tukio hilo wanalichukulia kama la kishirikina kwa sababu,
kabla ya kuku huyo kubeba pesa hizo, ilitokea hali ya tofauti eneo hilo
ambapo kulitokea kama ukungu ghafla na ndipo wanakikundi wakawa kama
wamepumbazwa ndipo kuku huyo akanyakua pesa hizo walizokuwa wameziweka
kwenye ungo.
Alisema
kuku huyo alikuwa mwenye rangi nyeupe, ambayo ni aina ya kuku
wanasemekana kuwa wanatumika sana katika nguvu za giza na hivyo
waliamini kuwa tukio hilo lilikuwa la kishirikina.
“Ilikuwa
majira ya saa 11 jioni, tulikuwa tumekaa tunapiga mahesabu ya pesa zetu
ili tugawane ndipo akatokea kuku mweupe aliyekuwa anarukaruka na
kusogea eneo tulipo, lakini sisi kwa sababu tumezoea kuwa kuku ni ndege
wa kawaida anayefugwa hatukuwa na wasiwasi”
“lakini
ghafla ilitokea kama ukungu, tukawa tumepumbazwa ndipo ghafla kuku huyo
akadonoa fedha zetu na kukimbia nazo,” alisema Kitaje.
Kwa
upande wake katibu wa kikundi hicho, Basimenye Silimmani, alisema kuwa
jumla ya fedha zote za kikundi hicho zilikuwa 2490,000 lakini na baada
ya kurudia mahesabu ili wajuwe kuku huyo alikuwa amebeba kiasi gani
ndipo walipobaini kuwa 430,000 hazipo.
Silimmani
alisema kuwa walishindwa cha kufanya baada ya tukio hilo lakini kwa
sasa wanamtegemea mungu kwa madai kuwa yeye ndiye aliyekuwa amewapatia
njiaza kupata fedha hizo na hivyo wanamtegemea yeye awalinde.
Hata
hivyo aliwataka wenzake kutokata tamaa na kwamba kwa kuwa wanamtegemea
mungu kikundi chao kitaendelea kuwa imara na kwamba kilichotokea ni
jaribu kama majaribu mengine.
Tukio
kama hili limekuwa la pili kutokea mkoani Mbeya mwezi huu ambapo
mwanzoni mwa mwezi huu lilitokea katika Kijiji cha Ibale kata ya Ibale
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ambapo mbwa alitokomea na pesa za
wanakikundi shilingi milioni 1 kati ya milioni 6 mkoani hapa
Ludewa yetu na maendeleo yetu