ome News Taarifa za Habari HAPO ZAMANI PALIKUWEKO BENDI INAITWA JAMHURI JAZZ BAND
Kwa
mara ya kwanza niliwaona ‘Live’, Jamhuri Jazz Band wakipiga katika
ukumbi wa Community Welfare Centre Iringa mwaka 1969, ukumbi huo
ulikuwa maarufu kwa wenyeji wakati huo kwa jina la Olofea senta (Welfare
Centre). Ulikuwa ukumbi ambao ulikuwa mali ya serikali. Katika miaka
hiyo, bendi ilikuwa ikipiga maonyesho mawili kwa siku, onyesho la kwanza
likiwa kati ya saa nane mpaka kumi jioni, likiwa haswa kwa watoto, na
lilijulikana kama ‘Buggy’, kisha dansi tena lilikuja kuanza saa 2-3
usiku likiwa maalumu kwa watu wazima tu. Wakati huo mwanafunzi hata kama
ni wa sekondari alichukuliwa kuwa ni mtoto na marufuku kuingia onyesho
la usiku. Ni vigumu kuelezea jinsi nilivyokuwa najisikia kwani nilikuwa
sidhani kama kutakuja kuweko na wanamuziki watakaoweza kupiga muziki
vizuri kuliko wale jamaa. Nilipenda mno kumuangalia mpiga rythm guitar
Harison Siwale, aliyejulikana kwa jina la Satchmo, alikuwa na anabakia
kuwa mpiga gitaa aliyenifurahisha kuliko wote. Na hakika mpaka leo
upigaji wake haukuwahi kuigwa. Ukisikiliza nyimbo kama vile Blandina,
Mganga no 1, Maria bembeleza mwana au Ewe ndege, utanielewa nabaki
kusifia kuwa huyu bwana alikuwa na kipaji cha pekee. Kuna rafiki yangu
aliwahi kumuuliza wakati ule huwa anapataje mawazo ya kupiga gitaa lake
kwa staili ile? Alijibu kuwa huwa anajaribu kupiga sauti za viumbe
mbalimbali wa porini katika gitaa lake.
Wanamuziki waliokuwa katika bendi ya Mkwawa High Schoolmiak hiyo , Manji, Sewando, Danford Mpumilwa, Askofu Kakobe watakumbuka jinsi walivyoweza kupata nafasi ya kupiga pamoja na bendi hii kila ilipokuja Iringa mjini, maana hizo ndiyo zilikuwa taratibu wakati huo lazima bendi kubwa ikija, wanamuziki wadogo huomba Kijiko, na kama unaweza kuimba au kupiga vizuri chombo fulani basi unaachiwa upige, na kama unafanya vizuri bendi iliweza hata kukuajiri. Bendi
ikifika katika mji, kama mji ule una bendi basi nao watapata nafasi ya kushirikiana na wageni. Jamuhuri Jazz band ilianza kwenye miaka ya 50 ikiwa ikijulikana kama Yanga Nyamwezi Band, Kiukweli ilikuwa ni Young Nyamwezi Band, bendi iliyokuwa imetengenezwa kwa ajili ya vijana toka Tabora waliokuja Tanga kufanya kazi ya kukata mkonge katika mashamba ya mkonge yaliyokuweko Tanga miaka hiyo. Na baada ya Uhuru ikajulikana kama Jamhuri Jazz Band, kifupi JJB japo kifupi hicho baadae kilidaiwa kuwa kilikuwa kifupi cha jina mwenye bendi Joseph Bagabuje. Wakati wa uhai wa Jamhuri Jazz bendi Tanga kulikuwa kuna waka moto kwa vikundi maarufu katika Afrika ya Mashariki kuwa vyote katika mji huo. Atomic Jazz, Amboni Jazz, Lucky Star, Black Star. Kwa vyovyote Tanga ulikuwa mji wa starehe wakati huo, hasa ukikumbuka kuwa kulikuweko na bendi nyingine ambazo hazikuwa m

Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment