HAWA NI WATUHUMIWA AMBAO NI ASKARI MGAMBO WALIOKUWA WAKILINDA BENKI YA WANANCHI NJOCOBA TAWI LA MAKAMBAKO
HILI NI GARI LA SOMA BIBLIA AMBALO WAMILIKI WAKE WALIIBIWA FEDHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI SABA NA LAKI NANE WAKATI WATUMISHI WAKE WAKIWA NYUMBA YA KULALA WAGENI MJINI NJOMBE ZURICHI GUEST HOUSE.
KAIMU KAMANDA WA JESHI LA POLISI MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI MKOA WA NJOMBE SSP JOHN TEMU AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
WAPO MIKONONI MWA POLISI HAPA WAMETIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI
KAIMU KAMANDA WA POLISI MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI MKOA WA NJOMBE JOHN TEMU
WATUHUMIWA WA WIZI WA MAFUTA HALFAN PETER NA STEPHEN KAIWAGA SASA WANAPELEKWA MAHABUSU
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linawashikilia Askari Mgambo Wawili Walinzi Wa Benki Ya Wananchi Njombe Njocoba Tawi La Makambako Kwa Tuhuma Za Kutelekeza Silaha Yenye Namba TZ CAR 39957 Aina Ya Short Gun Katika Eneo La Lindo Huku Wao Wakielekea Kuiba Mafuta Kwenye Magari Makubwa Yalioegeshwa Kwenye Barabara Inayoelekea Mbeya.
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Ofisini Kwake Kaimu Kamanda Mrakibu Mwandamizi Wa Polisi Mkoa Wa Njombe John Temu Amewataja Askari Mgambo Waliokamatwa Wakiwa Wametelekeza Silaha Hiyo Kuwa Ni Sephen Kaiwaga Maarufu Kama Lupenza Mwenye Umri Wa Miaka 32 Mkazi Wa Ilembula.
Aidha Kamanda Temu Amemutaja Mtuhumiwa Mwingine Kuwa Ni Halfan Peter Mkazi Wa Kitisi Makambako Wote Walinzi Wa Kampuni Ya Over Speed Security Guard Wanaolinda Katika Benki Ya Wananchi Njombe Tawi La Makambako Walikutwa Na Askari Wa Polisi Waliokuwa Kwenye Doria Wakiwa Wameacha Silaha Hiyo Na Kwenda Kuiba Mafuta Ya Diesel Kwenye Magari Ya Mizigo Yalioegeshwa Kando Ya Barabara Ya Kuelekea Mbeya.
Amesema Watuhumiwa Hao Walikutwa Na Gari Dogo Walilokodi Kwaajili Ya Shughuli Hiyo Lenye Namba T977APE Toyota Mack 11 Likiendeshwa Na Silvanus Lupenza Mkazi Wa Kahawa Makambako Tukio Ambalo Limetokea Januari 22 Majira Ya Saa Tano Na Dakika 45 Usiku Katika Mtaa Wa Mwembetogwa Makambako.
Katika Hatua Nyingine Kaimu Kamanda Huyo Mrakibu Mwandamizi Wa Polisi Mkoa Wa Njombe John Temu Amesema Jeshi La Polisi Linamshikilia Mkazi Mmoja Wa Ubungo Jijini Dar Es Salaam Abdully Salumu Mwenye Umri Wa Miaka 39 Kwa Tuhuma Za Kuiba Fedha Zaidi Ya Shilingi Milioni 7 Na Laki 8 Zilizokuwepo Kwenye Nyumba Ya Kulala Wageni Ya Zurichi Mjini Njombe.
Amesema Fedha Hizo Ambazo Ni Mali Ya Shirika La Soma Biblia Lenye Makao Yake Makuu Mwanjelwa Mkoani Mbeya Ziliibwa Baada Ya Wageni Wa Shirika Hilo Wanaojishughulisha Na Kuuza Biblia Kwenda Kulala Kwenye Nyumba Hiyo Ambapo Tukio Hilo Lililotokea Januari 21 Majira Ya Saa Mbili Na Nusu Usiku .
Kaimu Kamanda Wa Polisi Mrakibu Mwandamizi Wa Polisi Temu Amesema Mtuhumiwa Huyo Baada Ya Kuiba Fedha Hizo Alianza Kukimbia Ndipo Wananchi Walianza Kumkimbiza Huku Fedha Nyingine Akizitupa Chini Na Zilifanikiwa Kupatika Shilingi Milioni Tatu Na Laki Saba Ambapo Watuhumiwa Hao Wote Upepelezi Utakapo Kamilika Watafikishwa Mahakamani
Na ngilangwa ,Njombe
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment