Mlimani Park Orchestra ilianzishwa mwaka 1978 katika kitongoji cha Mwenge katika jiji la Dar. Thobias Chidumule ni mmojawapo ya wanamuziki waanzilishi wa bendi hii na alikuwa namna pekee ya utunzi na uandikaji wa nyimbo zake kwa namna ambayo alitaka kuwasilisha ujumbe kwa hadhira yake. Akionesha ukomavu wake kama vile mwalimu anavyoweza kufanya kwa wanafunzi wake tobias aliwagusa wengi kwa tungo zake na muziki safi. Nyimbo kama "Mtoto Akililia Wembe" na Usitumie Pesa Kama Fimbo" zinaonyesha namna ambavyo alikuwa na ueledi na falsafa ya hali ya juu ktk maisha. Hata hivyo bendi hii haikuwa maarufu mpaka Bichuka alipojiunga nayo miaka ya mwanzo ya 80. Hassan Bichuka alikuwwamtulivu na mwenye ushawishi mkubwa kwenye bendi. Sauti yake ni ya juu, tulivu na yenye kuleta utofauti na ya Tobias ambaye huimba kwa hisia kali za mwili na kuzihamishia kwenda kwenye sauti inayobadilika na kuwa ya juu. Pamoja na kuwa na sauti iliyotulia tungo za Bichuka ni za kimapenzi zaidi na kibinafsi tofauti na Tobias ambaye tungo zake zinajikita kisiasa zaidi. Baadhi ya tungo za Bichuka alipokuwa na Mlimani Park zinazopendwa zaidi ni 'fikirini nisamehe' na 'neema'. Neema uliweza kushika nafasi ya kwanza kama muziki bora wa mwaka kwa miaka miwili mfululizo (1985-1986). Wimbo huu unaonesha ukomavu wa utunzi wa nyimbo za kitanzania. Mwanamuziki mwenye kipaji zaidi katika bendi ni Michael Enoch, mpiga gita wa zamani wa Dar jazz band ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa bendi hiyo kabla hajahamia Mlimani Park Ochestra. Huyu ndiye hufanya maamuzi ya mwisho juu ya mpangilio wa muziki japo wanamuziki wengine nao wanaruhusiwa kukuonesha ubunifu wao. Si jambo la ajabu kumkuta Enoch akiwa jukwaani akiwaongoza wenzake kukung'uta gitaa la solo ktk nyimbo ambazo ameshiriki kuzipangilia. Kwa kawaida si rahisi kwa wanamuziki nguli kufanya kazi pamoja. Hivyo Tobias na Bichuka wamewahi kuihama bendi hii ktk vipindi tofauti na kurejea katika vipindi tofauti. Kwa sasa Bichuka yupo na Tobias hayuko tena na bendi hii. Hata hivyo pamoja na hayo muziki wa Mlimani Park utaendelea kusikika ktk kumbi mbalimbali za muziki Tanzania. Kuna albamu yenye mkusanyiko wa nyimbo za Mlimani Park toka Radio Tanzania inapatikana na si vibaya kujipatia nakala yako. |
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment