Prodyuza kutoka Norway, Carl Hovind.
Na Hashim Aziz
Ipo wazi kwamba mastaa wawili wakubwa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Diamond Platnumz na Ali Kiba hawapikiki chungu kimoja kutokana na kila mmoja kujiona yupo juu ya mwenzake, lakini hilo halimzuii prodyuza wa kimataifa kutoka Norway, Carl Hovind kufanya kazi na wawili hao ndani ya studio moja.
Carl, mmiliki wa studio kubwa ya Olyp iliyopo Oslo, Norway aliyewahi kufanyakazi na wasanii wakubwa wakiwemo Damian Marley, Christopher Martin, Busy Signal, Gyptian, Roberto (Amarula) na wengine wengi, katika mahojiano maalum na Showbiz, ameeleza sababu ya kuja Bongo kuwa ni kuhakikisha wasanii wa Bongo Fleva wanatusua kimataifa.
MSIKIE CARL
“Unaweza kudhani Diamond au Ali Kiba anafahamika sana kimataifa lakini ukweli ni kwamba ukiona anaenda kufanya shoo Ulaya, wengi wanaoingia ni Watanzania wanaoishi kule, nataka kuivunja laana hiyo. Nataka muziki wa Kitanzania ufanye maajabu kama alivyowahikufanya Psy wa Korea na wimbo wake wa Gangnam Style,” alisema Carl na kuongeza:
“Kikwazo kikubwa kinachowafanya wasanii wengi wa Bongo kutowika kimataifa, ni mfumo mbovu ambao upo kuanzia ngazi za chini kabisa mpaka serikalini. Wasanii hawawezeshwi kukua na kutoboa nje ya mipaka ya Tanzania. Angalau mwaka huu nimesikia wasanii wataanza kulipwa kadiri nyimbo zao zitakavyokuwa zinachezwa redioni, hiyo ni hatua ya kwanza lakini bado kuna mengi ya kufanya.
AMEPANGA KUFANYA NINI?
“Nimeshafanya mawasiliano na wasanii kadhaa Bongo wakiwemo Diamond, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Lady Jaydee, Kayumba wa BSS, Esco Dee na wengine wengi ambapo nitaingianao studio na kurekodi nao ngoma kali zenye hadhi ya kimataifa. Kisha baada ya hapo, nitasafiri kwenda Los Angeles kwenye studio zetu nyingine ambapo nitazifanyia mixing ngoma zote kisha nitaenda kumalizia kazi Oslo, Norway.
“Baada ya hapo, nitaanza kuachia ngoma moja baada ya nyingine na ambaye atabahatika kutoa hit kali ya kimataifa, tutaingia naye mkataba wa kumfanya awe staa mkubwa duniani,” alisema Carl na kuongeza:
“Nimepangapia kuonana na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye na kuzungumza naye jinsi serikali inavyoweza kuwajengea mazingira mazuri wasanii wake ili waweze kutambulika kimataifa.
VIPI KUHUSU GHARAMA ZA KUREKODI?
“Hakuna msanii anayeweza kunilipa gharama ninazotaka hapa Tanzania, sijisifii lakini ukweli ni kwamba mimi ni miongoni mwa maprodyuza ghali zaidi duniani. Kwa sababu lengo langu ni kusaidia, nitawarekodia bure wasanii wote, ninachotaka ni vipaji na ubunifu wenye levo za kimataifa.
“Kwa hao wasanii niliowataja, mipango inaendelea vizurilakini kama kuna wengine ambao wanadhani wanazo sifa na vigezo, wanaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kupitia ukurasa wangu wa Instagram wa jamproductions,” alihitimisha Carl.
Unaweza pia kupata mahojiano yake kupitia Global TV online kwa kubofya www.globaltvtz.com.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment