Yasutaro Koide enzi za uhai wake.
Mwanaume mzee kuliko wote duniani amefariki dunia leo jijini Nagoya nchini Japan akiwa na umri wa miaka 112.
Yasutaro Koide, kutoka Nagoya, alizaliwa Machi 13, 1903 na alitambuliwa na Guiness Book of World Records kama mwanaume mzee zaidi duniani Agosti mwaka jana.
Yasutaro amefariki kutokana na maradhi ya moyo na nimonia.
Enzi za uhai wake aliwahi kuulizwa siri ya mafanikio katika maisha yake ambapo aliwashauri watu wasivute sigara wala wasinywe pombe na waache kujiumiza sana na kazi na pia waishi kwa furaha.
Bado haijabainika ni nani atamrithi kama mwanaume mzee zaidi aliye hai duniani.
Mtu aliyeishi muda mrefu zaidi duniani kwa mujibu wa rekodi za Guinness alikuwa Mfaransa Jeanne Calment, aliyeishi miaka 122 na siku 164. Alifariki Agosti 1997.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment