Inakuwaje wakali wangu wa nguvu? Oya masela barida? Basi kipande hii haina kwikwi chaliiangu. Ni mpango mzima makachaa wangu.
Ebana maandalizi ya kitu cha mnuso wa Eksimasi kwani vepee? Maana kama sielewielewi f’lani hivi. Naona pipo wapo bize kinoma hata hatupeani michongo kama ishu inakuwaje wazazi? Bati freshi hata kama chama langu hana kitu masti kitu cha holidei kihapeni.
Tangu tulipomingo lasti wiki kumekrosi mambo kibwena hadi tudei tunamiti hapa kwa fasi ya jamvini. Wanangu Saa Godi mkubwa kinoma washkaji zangu. Kwa mkono wake tumefika kwenye X-masi tukiwa fiti kabisa! Dheni cha kufanya ni kumpigia goti. Ama nini? Basi barida! Kipande hiyo ishu zikoje makachaa? Maana sipati picha hilo bata linavyoliwa kijanja. Yap! Kijanja kozi ukitaka ulile kimbululambulula litakutokea puani. Pigeni mdogomdogo au kitorondo watu wangu wa nguvu la sivyo mtajikuta kwa masnichi wa difenda. Dheni tuanze kuhaha kukuchomoa nyuma ya nondo! Acheni hizo!
Nimekuwa na sistimu ya kuwasanua wana kuwa taimu inamuvu fasta kinoma na ukweli wa yestadei unaweza kuwa uongo mkubwa kinoma wa tudei na tumoro. Tunapiga kitu cha bata la maana bila kuharibu wanangu wenyewe.
Hapa sasa natoku na masela wangu wa kitaa ambao wamepania hizi bata za msimu wa holidei. Wale tunaohaso pamoko na kutanua kwa mkwanja halali ndo mpango mzima. Wale tunaosafa kinoma na hili laifu tukiwa apache alolo tumechalala si ndo tuna mahasira sasa ya kula bata letu bila kuzinguana? Ebana kama kuna mtu hana kitu kwa poketi bora akambonji skani kuliko kufosi kuvaa kiatu cha kushoto kwenye mguu wa kulia.
Achana na bata fekelo za magumashi. Unajua ukiwa na ngawira au mawe ambayo umefaindi bila magumashi hata matumizi yake huwa hayana kabisa mastresi. Sasa wewe umetafuta mkwanja halafu unatumia kwa kujificha kama mafisadi si haina utamu mazee? Kama vipi kwa wale tuliohaso tupige bata zetu za ukweli kiroho safi bila mizinguo,
Wanangu mmeshafunga mahesabu lakini? Yap! Huo ndo mpango usije ukapelekwapelekwa kama ling’ombe bila maplani. Kichwa timamu hakiendiendi tu bila daireksheni. Sasa si hiyo ndo fomula au taimu tebo? Kama bado sanuka wewe. Dunia ipo spidi unaachwa dakika ziro.
Mmenisoma wana? Sasa hilo bata wapi? Kama vepe sii yuu neksti wiki.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment