Hans Mloli,
Dar es Salaam
UNAWEZA kuona kama ni utani lakini ndiyo hali halisi ilivyo, Klabu ya Simba imeamua kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wao, Mserbia, Goran Kopunovic.
Dar es Salaam
UNAWEZA kuona kama ni utani lakini ndiyo hali halisi ilivyo, Klabu ya Simba imeamua kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wao, Mserbia, Goran Kopunovic.
Ishu ya kuanza mazungumzo na kocha huyo iliibuka wakati wa mchakato wa awali ulipoanza wa kumtafuta kocha msaidizi wa timu hiyo ambaye mpaka sasa bado hajapatikana baada ya kocha mkuu wa wekundu hao, Dylan Kerr kuchomoa ujio wa Mganda, Moses Basena.
Habari ikufikie kuwa Kopunovic ameshamaliza mazungumzo ya awali na vigogo wa timu hiyo siku chache kabla ya kurejea kwa Ligi Kuu Bara iliyokuwa imesimama kwa muda.
Taarifa kutoka ndani ya Simba inayoshikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi 23 baada ya mechi 11, inaeleza kuwa mazungumzo hayo yalikuwa na mlengo wa kusikiliza msimamo wa Kopunovic kama anaweza kurejea klabuni hapo msimu ujao awe kocha mkuu.
Mambo yamekwenda sawa na tayari Mserbia huyo amejumuishwa kwenye listi ya makocha wanaopewa kipaumbele kuja kuinasua timu hiyo msimu ujao mara baada ya kuondoka kwa Kerr anayetarajia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Ingawa Kerr amekuwa akifafanua mara kwa mara kuhitaji muda zaidi kwa ajili ya kuiweka sawa na kurejesha hadhi ya timu hiyo, lakini imedaiwa kuwa uongozi hauridhishwi na utendaji kazi wake, hivyo lolote sasa linaweza kutokea.
Kerr alitua Simba msimu huu baada ya kuondoka kwa Kopunovic aliyeshindwana na Simba dau la usajili wa mkataba wake mpya na ilielezwa kuwa alitaja dau kubwa baada ya kuonyesha angalau mwanga wa kuipeleka Simba inapopataka kufuatia kuinoa timu hiyo kwa miezi sita pekee.
“Mazungumzo na Kopunovic yamefanyika ila yamesimama baada ya kuafikiana mahala fulani, jinsi itakavyokuwa kulingana na mwenendo wa timu, Kopunovic ana asilimia kubwa ya kuja tena msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Rais wa Simba, Evans Aveva kuzungumzia ishu hiyo, simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila ya kupokelewa.
Alipotafutwa Rais wa Simba, Evans Aveva kuzungumzia ishu hiyo, simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila ya kupokelewa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment