VAN GAAL ATOA ‘SPEECH’ ATAKA UMOJA, MOURINHO AKISUBIRI
Ikiwa presha inazidi kuwa juu Manchester United, kocha Louis Van Gaal jana Jumatatu alitoa hutuba fupi iliyokua na hisia nzito hasa kutokana na mwenendo wa timu hiyo pamoja na tetesi za uwezekano wa kocha Jose Mourinho kutua Old Trafford kuchukua mikoba ya Van Gaal anayeonekana kushindwa kusongesha jahazi mbele.
Akiongea katika uwanja wa mazoezi wa Carrington huku akikabidhiwa zawadi ya maua ya Christmas na kushangiliwa na mashabiki wachache waliohudhuria tukio hilo, Van Gaal amesema, “sisi ni Manchester United, tutasonga mbele, lakini lazima tubakie wamoja, tushikamane”. Alisisitiza mholanzi huyo akiwahutubia wachezaji, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya mashabiki waliokuwepo.
Habari zinasema huenda Louis Van Gaal akafungishwa virago siku chache zijazo endapo tu atapoteza mchezo kati ya Stoke City ama Chelsea katika michezo ya ligi kuu soka England.
Manchester United tayari haijashinda katika michezo sita mfululizo huku ikipoteza michezo mitatu mfululizo, ikiwemo ule wa dhidi ya Norwich wikend iliyopita katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford na kuibua hasira za mashabiki ambao sasa waliowengi wanaonekana kumtaka Mourinho ambaye ametupiwa virago na Chelsea.
Gazeti la daily mail la nchini England limeripoti kuwa tayari maafisa wa Manchester United wamewasiliana na wakala wa kocha Jose Mourinho, mreno Gorge Mendez kumuweka tayari Jose Mourinho kwa ofa endapo klabu hiyo itaamua kumfukuza kazi Louis Van Gaal. Tayari Mourinho amewaambia rafiki zake kuvutiwa na kibarua cha kufundisha Manchester United
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment