Untitled
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Rais wa Shirikisho la Dunia la Soka (FIFA), Sepp Blatter (kushoto) na Rais wa UEFA, Michel Platini wamefungiwa miaka 8 kutojihusiaha na soka na kamati ya maadili ya FIFA kwa kosa la kutumia mamlaka yao vibaya kwa kosa la matumizi mabaya ya fedha za FIFA.
Blatter na Platini wanadaiwa kuwa mwaka 2011, kugawiana pesa kiasi cha Euro Milioni 1.35 ambapo Blatter alimlipa Platini kama malipo kwa kazi ya kuwa mshauri wa Blatter mwaka 1999-2002.
Licha ya kuwafungia miaka nane (8) pia wametozwa faini, Blatter akitakiwa kulipa faini ya Dolla 50,250 na Platini na Makamu wa Rais wa FIFA wakitakiwa kulipa faini ya Dolla 80,400.
Baada ya kutolewa kwa taarifa ya kifungo hicho, Rais wa FIFA, Sepp Blatter ametoa taarifa kuwa hakubaliani na hukumu hiyo na atakwenda katika mahakama ya michezo (CAS).
“Kufungiwa miaka 8 kwa kosa lipi?, nitapambana, nitapambana mpaka mwisho nimekuwa nikisaidia kupeleka soka mbele lakini leo napewa kifungo kikubwa kiasi hiki, nimechukua uamuzi nitakwenda kwenye mahakama inayohusika na michezo,” alisema Blatter katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Baada ya kifungo hicho kitakuwa kimefikisha kikomo cha uongozi wa Blatter katika Shirikisho la Soka Duniani FIFA ambapo amelitumikia kwa miaka 40 na 17 akiwa kama rais.