Habari ambazo sio rasmi zinadai kwamba kocha mkuu wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba Dylan Kerr hali yake kwenye klabu hiyo inafananishwa na ile ya kocha wa Manchester United Lois van Gaal kwasababu kocha huyo wa ‘mnyama’ amepewa mechi moja dhidi ya Mwadui FC ambayo kama atapoteza mchezo huo basi kibarua chake kitafika kikomo ndani ya Simba.
Kocha huyo mwenye asili ya England alianza majukumu ya kukinoa kikosi cha Simba kabla ya msimu huu kuanza na amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi 11 akipata ushindi kwenye kwenye michezo saba, sare mbili na amepoteza michezo miwili.
Klabu ya Simba kwasasa ipo nafasi ya nne kiwa na ponti 23 ikitanguliwa na Mtimbwa Sugar ambayo ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 24 wakati Azam inakamatia nafasi ya pili kwa pointi 29 huku wapinzani wao wa jadi Yanga wakiwa kileleni mwa VPL kwa pointi 30 tofauti ya pointi saba na Simba.
December 26, 2015 Simba itachuana na Mwadui FC ambapo matokeo ya ushindi ndiyo yatakuwa faraja pekee kwa kocha huyo lakini kama itakuwa vinginevyo uongozi wa klabu hiyo unaweza ukachuku uamuzi wa kusitisha mkataba wa kocha huyo.
Hali ya Kerr ndani ya Simba inafananishwa na ile ya kocha wa Manchester United Lois Van Gaal ambaye yuko kwenye presha kubwa baada ya kushindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye mechi sita huku zikiwepo taarifa kwamba wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazer pamoja na kaimu mtendaji mkuu Ed Woodward wanaamika tayari wameanza mazungumzo na wakala wa Jose Mourinho ambaye wiki iliyopita alitupiwa virago kwenye klabu ya Chelsea.
Simba ilitoka sare ya kufungana kwa goli 1-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza kwenye mechi iliyopita ikiwa ni sare ya pili mfululizo baada ya ile ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya Azam FC iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment