Ushindi walioupata Arsenal dhidi ya Manchester City umewapa imani kuwa wapo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu England msimu huu, amesema manager wa klabu hiyo Arsene Wenger.
The Gunners hawajatwaa taji la ligi kuu England tangu mwaka 2004, lakini magoli kutoka kwa Theo Walcott na Olivier Giroud yalitosha kuimaliza City licha ya Yaya Toure kufunga goli pekee kwa klabu yake dakika za lala salama.
“Inatufanya tujiamini, tunapata nguvu na imani”, alisema Wenger.
“Sasa angalau kikosi chetu kinajielewa, kitu ambacho unaweza kukiona wakati wa mchezo wakati tulipokuwa kwenye presha”.
Sasa Arsenal wako pointi nne mbele ya Manchester City lakini bado wanasalia nafasi ya pili pointi mbili nyuma ya vinara Leicester City.
Wakati huo mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya 15 na wanaonekana wako nje ya kinyang’anyiro cha ubingwa cha kutwaa ubingwa wa EPL huku nafasi kubwa wakipewa The Gunners.
Arsenal haijafungwa kwenye mechi sita mfululizo na hiyo inatoa matumaini kwa kocha wa kikosi hicho mzee Wenger ambaye anaamini msimu huu wanatakiwa kutwaa taji hilo walilolikosa kwa muda mrefu sasa.
“Miaka miwili au mitatu iliyopita tulikaa kileleni kwa muda mrefu lakini kitu special msimu huu ni kwamba, tumecheza bila wachezaji wetu wengi muhimu, tulisafiri kuwafuta Olympiakos, tukacheza dhidi ya Aston Villa na Man City lakini tumeshinda michezo yote”, amesema Wenger.
“Hicho ni kitu kizuri. Ninaimani kwamba tumeonesha vipaji vyetu na ari pamoja na kiwango cha juu ambavyo vimetupa pointi tatu”.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment