Klabu ya Chelsea inaamini staili ya maisha ya London itakuwa ni sehemu ya kigezo kikibwa cha kumnasa Pep Guardiola wakati wakijiandaa kutoa kitita kikubwa cha pesa kuwapiku Manchester City.
Roman Abramovich bado hajakata tamaa kumuwania Guardiola ambaye alilitosa dili la kujiunga na Chelsea mwaka 2012 na sasa ameshaweka wazi kwamba ataachana na Bayern Munich baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika.
City ndiyo klabu pekee kwa sasa ambayo inapewa nafasi kubwa ya kumshusha Guardiola jijini Manchester lakini bilionea wa Chelsea anataka kumfanya Guardiola si kocha atakayekuwa analipwa vizuri duniani bali yuko tayari pia kutoa kitita kikubwa cha pesa kwa kocha huyo kununua wachezaji ambao atawahitaji.
Abramovich anasubiriwa kutoa kauli yake baada ya kumtimua Jose Mourinho ambaye ni kocha mwenye mafanikio makubwa kwenye historia ya klabu ya Chelsea kwa kumdondosha kocha mwenye jina kubwa duniani.
Lakini wanafahamu fika kuwa si pesa pekeyake ambazo zitamfanya Guardiola kutua Chelsea pia wanaamini mke wa kocha huyo Cristina Serra anapendelea kuishi kwenye jiji la London baada ya kuondoka Munich.
Mmiliki wa Chelsea alikuwa akimlipa Jose Mourinho mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki sawa na pauni milioni 12 kwa mwaka kabla ya kumtimua Alhamisi iliyopita, anamwaga pesa kwa Guardiola kujaribu kumshawishi kuipa kisogo Manchester City.
Guardiola ameshaifanyia uchambuzi klabu ya Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa taji la EPL na amebainin inahitaji kusajili wachezaji 10 wapya.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment