Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter pamoja na Rais wa UEFA Michel Platini wamefungiwa kwa muda wa miaka nane (8) kujihusisha na masuala yoyote yanayo husu mpira wa miguu baada ya uchunguzi wa maadili dhidi yao kukamilika, hii ni kwa mujibu wa Kamati ya Maadili ya kujitegemea ya FIFA.
Wawili hao kwa pamoja walifungiwa kwa muda mwezi Oktoba, baada ya kuhusishwa na matumizi mabovu ya kiasi cha Euro milioni 1.34 za FIFA ambazo ziliidhinishwa na Blatter mwenyewe na Platini mwezi Februari 2011.
Hata hivyo, katika chapisho la siku ya Jumatatu, maamuzi yaliyofikiwa na Kamati ya Maadili meeleza kuwa malipo hayo hayakuwa na uhalali kutokana na kutokuwepo kwa hati ya makubaliano iliyosainiwa na maafisa wote mnamo Agosti 25, 1999.
Na zaidi ya hapo ni kwamba, utetezi wa Blatter juu ya makubaliano ya mdomo “ulichukuliwa kama usio na ushawishi na ulitupiliwa mbali na chumba cha hukumu (chamber)”.
Blatter (79), ambaye alishatangaza kuachia madaraka kama rais wa FIFA ifikapo February na kuitisha uchaguzi mpya wa rais, amepigwa faini ya Francs za Uswizi 50,000, huku Platini akipigwa faini ya Francs za Uswizi 80,000.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment