Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete akiungana na
wananchi wa Handeni Mkoani Tanga, katika kumzika aliyekuwa waziri wa
Viwanda na Biashara Dk. Kigoda, Rais akiwa na chepe ya mchanga.
Makamu
wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal ameongoza waombolezaji kuuaga mwili wa
aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara Dr.Abdalah Kigoda kabla ya
kusafirishwa kuelekea Handeni mkoani Tanga kwa maziko.
Zoezi
hilo limefanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali wakiwemo
marais wastaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, spika wa
bunge mama Anne Makinda na katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue.
Akitoa
salaam za serikali waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mathias Chikawe
mbali na kuelezea namna marehemu Kigoda alivyolitumikia taifa kwa
uadilifu katika nafasi zote alizopewa au kuteuliwa amesema wananchi wa
jimbo lake la Handeni wamepoteza kiongozi shupavu.
Baadhi
ya mawaziri na makatibu wakuu ambao aliwahi kufanya nao kazi nao
wamepata fursa ya kuelezea utendaji wake ambao wamedai kuwa ulikuwa
shirikishi jambo ambalo ni nadra kwa baadhi ya viongozi.
Mkurugenzi
mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi TPSF Bw Godfrey Simbeye ni
miongoni mwa viongozi wa taasisi zilizohudhuria zoezi hilo ambapo
amesema kwa niaba ya TPSF wamtaka rais ajaye na serikali ijayo
kuhakikisha inateua waziri wa viwanda na biashara atakayefuata nyayo za
marehemu Kigoda ambaye alipenda kujadiliana na sekta binafsi.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment