Mgombea
wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema, anayeungwa mkono na vyama
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Edward Lowassa ameitaka
tume ya uchaguzi kuhakikisha inafanya shughuli zake kimamilifu na bila
kupendelea upande wowote kwani kushindwa kufanya hivyo ni kuliingiza
taifa kwenye machafuko.
Mgombea
huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ametoa onyo hilo kali kwa tume
ya uchaguzi nchini katika siku yake ya mwisho ya kampeni kanda ya ziwa.
Wakati
siku za kuelekea Oct 25 zikizidi kuhesabika kwa haraka zaidi, Freeman
Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema taifa ambaye amesema watakaa umbali wa
mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupigia kura, wasubiri matokeo
yatangazwe hata kama ni kesho yake asubuhi.
Uchaguzi wa Tanzania unatazamwa na dunia kwa jicho la tatu kwasasa,
Viongozi
wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wakiongozwa na mgombea nafasi ya
urais Edward Lowasa wametuma salama za rambi rambi kwa familia Dkt
Emanuel Makaidi aliyefariki dunia.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment