Idadi
ya wagombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu, waliofariki wakiwa
kwenye harakati za kampeni imefikia sita, kufuatia kifo cha aliyekuwa
mgombea wa Ludewa (CCM) Deo Fikunjombe.
Wagombea wengine wa ubunge wa CCM waliofariki ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani.
Kombani alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu nchini India kutokana na ugonjwa wa saratani ya kongosho.
Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda , aliyefariki Oktoba 12, mwaka huu nchini India.
Dk.Kigoda ambaye alikuwa mgombea ubunge Jimbo la Handeni alizikwa Alhamisi wiki hii nyumbani kwake Handeni mkoani Tanga.
Kwa upande wa vyama vya upinzani waliofariki ni Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk Emanuel Makaidi.
Dk.Makaidi
ambaye alifariki juzi kutokana na maradhi ya shinikizo la damu alikuwa
akigombea ubunge jimbo la Masasi mkoani Lindi.
Wengine ni mgombea ubunge wa ACT jimbo la Arusha Mjini Estomih Malla na mgombea wa Chadema jimbo la Lushoto Mohammed Mtoi.
Mtoi alifariki katika ajali ya gari iliyotokea mwezi uliopita.
Kwa
mujibu wa kifungu namba 49 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985, iwapo
kutatokea kifo cha mgombea wa udiwani au ubunge na msimamizi wa uchaguzi
akajiridhisha, kampeni zitaahirishwa kwa siku 30 ili kupata mgombea
mwingine.
CHANZO: NIPASHE
RAHA YA MILELE UWAPE Eee BWANA....
NA MWANGA WA MILELE UWANGAZIE Eee BWANA....
WAPUMZIKE KWA AMANI................AMINA.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment