Mahakama ya juu visiwani Maldives, imebatilisha hukumu ya kifo kwa kupigwa mawe mwanamke anayeshukiwa kupata mimba nje ya ndoa.
Mahakama kuu ilikuwa imemhukumu mwanamke huyo kufa kwa kupigwa mawe kwa kupatikana na hatia ya uzinifu chini ya sharia .
Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama moja katika kisiwa maarufu kwa watalii na wanandoa cha Gemanafushi.
Mahakama
ya juu hata hivyo imetoa hukumu mpya inayobatilisha uamuzi wa hapo jana
ikisema kuwa sheria na kanuni za kimsingi zilikiukwa na mahakama ya
chini.
Mabadiliko
ya kikatiba nchini humo ilikuanisha sheria ya taifa hilo na sheria kali
kwa misingi ya dini ya kiislamu 'Sharia'imeipa mahakama nchini humo
uwezo mkubwa wa kutoa adhabu.
Adabu hi yo kupigwa kwa mawe hadi kufa ni hukumu ya kwanza japo mahakama imekuwa ikitoa adabu ya kuchapwa viboko hadharani.
Marufuku
hiyo ya kutoshiriki zina hata hivyo haiathiri watalii na wanandoa
wanaopenda kusafiri kisiwani humo kwa ajaili ya fungate.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment