wananchi wilayani
makete mkoani njombe wamekuwa na sintofahamu juu ya mkanganyiko juu ya umbali
wa kusimama baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu na kauli iliotolewa na
tume ya taifa ya uchaguzi ya kurudi nyumbani baada ya kupiga kura.
wakizungumza katika
kipindi kinachorushwa na redio green fm
91.5 Mhz.iliopo wilayani makete mkoani njombe,wananchi hao wameonesha
kuchanganywa na taarifa za tume kwa kuwa sheria inasema baada ya kupiga kura
unatakiwa kusimama umbali wa mita 200 bila kueleza nini unatakiwa kukifanya
baada ya umbali huo.
taarifa ya hivi
karibu ya tume ya taifa ya uchaguzi imekuwa ikisisitiza baada ya kupiga kura unatakiwa kurudi
nyumbani kuendelea na majukumu yako huku wakiaminishwa kuwa mawakala na
wasimamizi wa uchaguzi ndio watakuwa walinzi wa kura hizo.
mtangazaji wa kipindi
hicho cha Morning Alarm ya Green fm,Asukile Mwalwembe na Edwin Moshi
wamelazimika kukata kauli hiyo kwa kumpigia simu msimamizi wa uchaguzi
halmashauri ya wilaya makete bw.Emanueli Gregory huku swali la kwanza likiwa
''Nini mpiga kura anatakiwa kukifanya baada ya kupiga kura''??
''ahsante mtangazaji
niseme kwamba siku hiyo ni siku nyeti sana hapa nchini tarehe 25 oktoba mwaka
huu yaani jumapili hii,mandiki ya uchaguzi ni kuwa ukisha piga kura ukae umbali
wa mita 200 lakini tunasimamia kauli ya tume ya uchaguzi ya taifa NEC ukisha
piga kura rudi nyumbani kaendelee na shughuli zako na muda wajioni ukifika
kuanzia saa kumi kaa mbali mita 200 subili matokeo ambayo yatabandikwa katika
kituo hicho ulichopigia kura.''
matokeo ya uchaguzi
yatakusanywa ngazi ya kata ambapo matokeo ya udiwani yatatangazwa na msimamizi
wa uchagzui wa kata ,matokeo ya ubunge yatakusanywa na kutangazwa na msimamizi
wa jimbo husika .
bw.gregory ametumia fursa hiyo kuwataka
mawakala wa vyama vya siasa waliokula kiapo kuwa waaminifu na kuhakikisha
wanalinda kura za wagombea wao ipasavyo ili kuepusha machafuko na uvunjifu wa
amani.
pia amesema kuwa ni
vyema wapiga siku ya jumapili ya tarehe 25 oktoba mwaka huu kuto vaa sare au
aina yoyote ile inayoashiria chama fulani kwani siku hiyo akivaa sheria
itachukua mkondo wake kwa kuwa atakuwa anaendeleza kampeni za chama wakati muda
umeisha.
hata hivyo amekataa
mikusanyiko ya watu katika maeneo ya vituo vya kupigia kura wakati wote
wakusubili matokeo ya uchaguzi kwa kuwa ni kinyume cha sheria za uchaguzi.
MUNGU IBARIKI
TANZANIA,MUNGU WABARIKI WAPIGA KURA NA UTULIVU NA AMANI ITAWALE WAKATI HUU WA
UCHAGUZI.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment