Ole Sendeka Akerwa na Tabia ya Vijana Kupiga Deki Barabara Ili LOWASSA Apite
Mjumbe
wa kamati ya kampeni ya chama cha Mapinduzi, Christopher Ole Sendeka
amelaani kitendo cha mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kuruhusu
vijana kusafisha barabara ya lami ili msafara wake upite akidai kuwa
huo ni utumwa.
Ole
Sendeka alitoa kauli hiyo jana wakati akiwa katika mkutano wa
kumnadi mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan mjini Geita.
Juzi
mjini Musoma na jana Jijini Mwanza walijitokeza vijana na kupiga deki
barabara ili Lowassa apite, wakisema hawataki apate mafua.
Sendeka jana alikemea kitendo hicho katika mikutano kadhaa mkoani Geita akisema, “Lowassa
anatumia umaskini wa vijana wetu kuwalipa fedha ili wamwage maji kwenye
barabara ya lami kusafisha barabara msafara wake upite. Huo ni utumwa
si utumwa?” aliuliza Sendeka na kujibiwa na wananchi kwa sauti, “Ni utumwa.”
“Namtaka
Lowassa asitumie nafasi yake ya ugombea urais kudhalilisha utu wa
vijana kwa sababu ya fedha zake, tena ambazo hakuzipata kihalali
kuwalipa vijana wetu eti wakamsafishie barabara ya lami apite,”alisema.
Sendeka alisema kitendo hicho cha aibu kimeona matairi ya gari la Lowassa yana thamani kuliko utu wa vijana.
“Kama
kweli hakufadhili mpango huo wa kulipa vijana wafanye hivyo kwa nini
hakuwakataza alipoona wanamwaga maji ili msafara wake upite,” alihoji.
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/10/ole-sendeka-akerwa-na-tabia-ya-vijana.html#sthash.WlgEfNFY.dpuf
Ole Sendeka Akerwa na Tabia ya Vijana Kupiga Deki Barabara Ili LOWASSA Apite By Edwin Moshi at Tuesday, October 13, 2015 Mjumbe wa kamati ya kampeni ya chama cha Mapinduzi, Christopher Ole Sendeka amelaani kitendo cha mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kuruhusu vijana kusafisha barabara ya lami ili msafara wake upite akidai kuwa huo ni utumwa. Ole Sendeka alitoa kauli hiyo jana wakati akiwa katika mkutano wa kumnadi mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan mjini Geita. Juzi mjini Musoma na jana Jijini Mwanza walijitokeza vijana na kupiga deki barabara ili Lowassa apite, wakisema hawataki apate mafua. Sendeka jana alikemea kitendo hicho katika mikutano kadhaa mkoani Geita akisema, “Lowassa anatumia umaskini wa vijana wetu kuwalipa fedha ili wamwage maji kwenye barabara ya lami kusafisha barabara msafara wake upite. Huo ni utumwa si utumwa?” aliuliza Sendeka na kujibiwa na wananchi kwa sauti, “Ni utumwa.” “Namtaka Lowassa asitumie nafasi yake ya ugombea urais kudhalilisha utu wa vijana kwa sababu ya fedha zake, tena ambazo hakuzipata kihalali kuwalipa vijana wetu eti wakamsafishie barabara ya lami apite,”alisema. Sendeka alisema kitendo hicho cha aibu kimeona matairi ya gari la Lowassa yana thamani kuliko utu wa vijana. “Kama kweli hakufadhili mpango huo wa kulipa vijana wafanye hivyo kwa nini hakuwakataza alipoona wanamwaga maji ili msafara wake upite,” alihoji
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.