Kijana
mmoja aliyetambulika kwa jina la Juma Rajabu, 23, mkazi wa Kijiwe Samli
Wilaya ya IIala, Dar nusura auawe baada ya kula kichapo maeneo ya
Buguruni Sheli, hali iliyofanya afikishwe na polisi Hospitali ya Amana
jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Chanzo
chetu kilisema kijana huyo alipigwa hadi kupoteza fahamu na wabaya wake
waliodai kuwa aliwaibia na baada ya kichapo waliamini kuwa amefariki
dunia.
“Vijana
wale baada ya kumpiga naye kupoteza fahamu wakajua kuwa wamemuua, hivyo
wakamuacha palepale hadi polisi wa doria walipofika na kumchukua,”
kilisema chanzo ambacho hata hivyo haikuelezwa alituhumiwa kuiba nini.
Habari
zinasema baadhi ya watu wanaomfahamu kijana huyo walifikisha habari
nyumbani kwao wakidai kuwa ameuawa na maiti yake ipo Hospitali ya Amana,
hivyo maandalizi ya mazishi yakafanyika.
“Jumamosi
asubuhi familia yao baada ya kupata taarifa za ‘msiba’ waligawana
majukumu, wapo waliokwenda kuchumba kaburi, wapo waliokwenda kununua
sanda na upishi wa chakula ulifanyika,”alisema mama mzazi wa kijana
huyo aliyejitambulisha kwa jina la Tatu Mohamed (65).
Bi
Tatu alisema kila aliyepewa jukumu lake lilifanya na waliokwenda
Hospitali ya Amana walipofika walimkuta Juma akiwa hai ila akiwa
ameumizwa na kushonwa nyuzi kadhaa sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Watu
waliokwenda Amana walituarifu kwa simu kwamba Juma hajafariki dunia,
hivyo shughuli za msiba zikasitishwa mara moja na watu wakatangaziwa na
wakatawanyika.
Alipohojiwa na gazeti hili Juma alisema kuwa alipigwa na na watu asiowajua baada ya kusingiziwa kuwa ni mwizi.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko