Idara
ya elimu sekondari wilaya ya Makete mkoani Njombe umeahidi kutatua
changamoto zilizozua mvutano uliokuwepo kati ya wanafunzi wa kidato cha
tano na sita wa shule ya sekondari Lupalilo na uongozi wa shule hiyo
kufuatia hali iliyokuwa imejitokeza juzi majira na saa mbili usiku kwa
wanafuzi hao kuandamana hadi ofisi za kijiji cha Tandala kushinikiza
kutatuliwa matatizo yao.
Moja
ya madai yao ilikuwa ni pamoja kuutaka uongozi wa shule hiyo
kuwatenganisha vyumba vya kulala na wanafunzi wa vidato vya chini
“O-Level” kutokana na changamoto kadhaa wanazozipata ikiwemo kuwapigia
kelele na kulala watu wawili kitanda kimoja jambo ambalo hawalitaki.
Wakizungumza
na mwandishi wetu kwa masharti ya kutopigwa picha, kurekodiwa wala
kutajwa majina, wanafunzi hao wamesema wamekuwa wakitoa malalamiko
mbalimbali kwa uongozi wa shule bila kuona hatua zozote zikichukuliwa,
kabla ya juzi usiku kwenda kwa mkuu wa shule kudai madai yao hayo na
wakaishia kuambiwa waondoke shuleni hapo
Akizungumzia
suala hilo Afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Jacob Meena amesema
mara baada ya kuyasikiliza madai yao hatua stahiki zitachukuliwa ili
kulimaliza tatizo hilo mapema iwezekanavyo.
Na
ameyasema hayo hapo jana kabla ya kuingia kwenye kikao cha usuluhishi
ambacho mwandishi wa eddy blog hakuruhusiwa kushiriki kwa sababu za
kimaadili ya taratibu za shule hiyo
Mkuu
wa shule ya Sekondari Lupalilo Bw.Johnes Liombo amesema wameyapokea
madai hayo na kuahidi kuyafanyia kazi huku akiwasihi wanafunzi hao
kufuata sheria na taratibu za shule.
Kwa
upande wake diwani mstaafu wa kata ya Tandala Egnatio Mtawa ambaye
wanafunzi hao walipoandamana juzi walihitaji kuzungumza naye na si mtu
mwingine, akamweleza afisa elimu sekondari wilaya jinsi hali ilivyokuwa
hapo juzi na hatua alizozichukua ikiwemo kuwarudisha shuleni kwa ajili
ya kulala baada ya kuzungumza nao usiku huo, na kuongea na mkuu wa shule
pamoja na afisa elimu sekondari kwa kuwapigia simu ili wakutane pamoja
jana kutatua mgogoro huo
Naye
mkuu wa kituo cha polisi Tandala Inspekta Majiruka amewataka wanafunzi
kutulia na kutojiingiza katika vurugu zozote ikiwemo kuharibu mali za
shule wakati taratibu za kuyatafutia ufumbuzi matatizo yao zikiwa
zinaendelea.
Hadi
tunachapisha habari hii, kilikuwa kikiendelea kikao cha kuumaliza
mgogoro huo kilikuwa kinaendelea kikiongozwa na afisa elimu sekondari
wilaya ya Makete ambapo haikuruhusiwa waandishi wa habari kushiriki
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko