Huenda ukawa unajiuliza Neymar atakuwa wapi katika mapumziko haya mafupi kwa Ligi mbalimbali duniani, baada ya kutojumuishwa katika kikosi cha Brazil kutokana na kuendelea kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika michuano ya Copa America, kadi iliyopelekea kufungiwa mechi nne ambazo hadi sasa ametumikia mbili kati ya hizo.
Neymar ambaye hakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilichofungwa na Chile goli 2-0, mechi iliyochezwa ijuma ya October 9. Neymar katumia muda wa mapumziko kuenjoy na marafiki zake kwa kutoka maeneo tofauti tofauti.
Staa huyo wa FC Barcelona ya Hispania ameonekana katika pati ya mtaani mjini RioDJaneiro Brazil akiwa na waigizaji wa kibrazil wakiwemo Rafael Zulu, Caio Castro, Thiago Martins na ‘Queen of the Carnival’ Paloma Bernardi. Neymar alifungiwa mechi nne baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa Colombia katika michuano ya Copa America.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment