Bado uhamisho wa mshambuliaji wa zamani wa FC Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Hispania Pedro Rodriguez kujiunga na Chelsea unaendelea kuwaumiza wachezaji wenzake wa zamani, baada ya Daniel Alves kusema kuwa ni bora nyota huyo angeendelea kubakia FC Barcelona kuliko kujiunga na Chelsea.
“nilimwambia
Pedro asiondoke FC Barcelona lakini kulikuwa na watu wengi waliohusika
katika hili, kama angebakia FC Barcelona angeendelea kuwa na furaha
hapa, lakini hatukuwa katika nafasi ya kufanya maamuzi kuhusiana na
mpango huo kama tungekuwa na nafasi ya kufanya hivyo ningependa abaki
hapa kwa miaka mingi zaidi”>>> Alves
Pedro Rodriguez aliamua kuhama na kujiunga na klabu ya Chelsea ya Uingereza kwa dau la pound milioni 22, baada ya kupoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha FC Barcelona. Pedro ilimlazimu kuondoka kutokana na nafasi yake ya kucheza kuwa finyu kutokana na uwepo wa Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar kuwa wanafanya vizuri wakicheza pamoja.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment