MARTIAL AKIANZA MECHI YAKE YA KWANZA KWA FRANCE


FRANCE-MARTIAL-GIROUDCHIPUKIZI wa Mika 19 wa Manchester United Anthony Martial Jana alianza Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Nchi yake France ilipoichapa Denmark 2-1 katika Mechi ya Kirafiki nay eye kung’ara mno.
Licha ya yeye kutofunga Bao katika Mechi hiyo iliyochezwa huko na Bao za France kufungwa na Straika wa Arsenal, Olivier Giroud, ndani ya Dakika 6 za kwanza lakini yeye alitengeneza Bao la kwanza kwa kasi na ujanja wake.
Katika Mechi hiyo, Martial alicheza upande wa Kushoto na kudumu Dakika 87 kabla hajatolewa na kupumzishwa.
Martial, akicheza nyuma ya Straika mkuu wa France Giroud, alishaini kwa spidi yake na kuichambua Difensi ya Denmark kwa maarifa makubwa yanayozidi umri wake wa Miaka 19.
Katika Dakika ya 62, Martial aliikata Difensi ya Denmark na kumtambuka Lars Jacobsen na kukutana ana kwa ana na Kipa Kasper Schmeichel lakini Shuti lake liliokolewa na Kipa huyo anaedakia Leicester City.
Kocha wa France, Didier Deschamps, ameonyesha kuridhishwa na maendeleo ya Martial ambae alinunuliwa na Man United Septemba 1 kutoka AS Monaco na kudokeza kinda huyo ni mmoja wa Wachezaji wake wa Fainali za EURO 2016 zitakazochezwa Mwakani ambazo France ndio Wenyeji.



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: