EURO 2016: GERMANY, POLAND, ALBANIA, ROMANIA ZATINGA FAINALI



EURO2016JANA Germany, Poland, Albania na Romania zimeungana na Nchi nyingine 12 kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, zitakazochezwa Mwakani huko France.
Nchi nyingine ambazo zilifuzu mapema ni 12 na kufanya Jumla ya Timu 16 zilizofuzu hadi sasa na kubakisha Nafasi 8 ambazo 4 zitajazwa moja kwa moja toka Mechi zilizobakia za Makundi zitakazochezwa Leo na Jumanne wakati 4 za mwisho zitatokana na Mechi Maalum za Mchujo zitakazoshirikisha Timu 8 zitakazomaliza Nafasi za 3 za Makundi yao.
Nchi zilifuzu mapema ya Jana ni Wales, Belgium, Italy, Austria, the Czech Republic, England, Wenyeji France, Iceland, Northern Ireland, Portugal, Spain na Switzerland.
Hapo Jana, Mabingwa wa Dunia Germany walisota kuupata ushindi wa Nyumbani wa 2-1 walipocheza na Georgia na kufanikiwa kutinga Fainali za EURO 2016 toka Kundi D pamoja na Poland ambao nao walishinda Nyumbani kwa kuibwaga Republic of Ireland 2-1.
Germany, wakihitaji Sare tu, waliifunga Georgia 2-1 kwa Penati ya Thomas Muller iliyosawazishwa na Jaba Kankava lakini Dakika ya 79 Max Kruse akawapa Bao la ushindi.
Nao Poland waliichapa Republic of Ireland 2-1 kwa Bao za Grzegorz Krychowiak na Robert Lewandowski huku Bao la Republic of Ireland likifungwa na Jon Walters.
Bao la Lewandowski limemfanya afikishe Bao 13 katika kampeni moja ya EURO na kumfanya aungane na Straika wa Northern Ireland, David Healy, ambae nae alipiga Bao 13 katika Mashindano ya EURO kwa kampeni moja.
Nao Albania wametinga Fainali zao za kwanza za Mashindano makubwa baada ya kuichapa Armenia 3-0 pamoja na Romania ambao nao waliitwanga Faroe Islands 3-0 na kutinga Fainali za EURO 2016.


 MATOKEO:
Jumapili Oktoba 11
Armenia 0 Albania 3
Faroe Islands 0 Romania 3
Finland 1 Northern Ireland 1
Greece 4 Hungary 3
Serbia 1 Portugal 2
Germany 2 Georgia 1
Gibraltar 0 Scotland 6
Poland 2 Republic of Ireland 1
TIMU ZILIZOFUZU HADI SASA [16 bado 8]:
-France [Wenyeji]
-KUNDI A: Iceland, Czech Republic
-KUNDI B: Belgium, Wales
-KUNDI C: Spain
-KUNDI D: Germany, Poland
-KUNDI E: England, Switzerland
-KUNDI F: Northern Ireland, Romania
-KUNDI G: Austria
-KUNDI H: Italy
-KUNDI I: Portugal, Albania
EURO 2016
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumatatu Oktoba 12
1900 Austria vs Liechtenstein
1900 Russia vs Montenegro
1900 Sweden vs Moldova
2145 Belarus vs Macedonia
2145 Estonia vs Switzerland
2145 Lithuania vs England
2145 Luxembourg vs Slovakia
2145 San Marino vs Slovenia
2145 Ukraine vs Spain
Jumanne Oktoba 13
2145 Belgium vs Israel
2145 Bulgaria vs Azerbaijan
2145 Cyprus vs Bosnia and Herzegovina
2145 Italy vs Norway
2145 Latvia vs Kazakhstan
2145 Malta vs Croatia
2145 Netherlands vs Czech Republic
2145 Turkey vs Iceland
2145 Wales vs Andorra


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: