JAKAYA MRISHO KIKWETE YOUTH PARK YAKARIBISHA VIJANA KUPIGA MECHI

JAKAYAKIKWETE-YOUTHPARKUONGOZI wa Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park umetoa mwaliko kwa Vijana wote na Watanzania kwa ujumla kwenda kutumia Eneo hilo jipya na la kisasa kabisa.
Uwanja huo upo Kidongo Chekundu katikati ya Jiji la Dar es Salaam na umejengwa kutokana na kuhudi kubwa za Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na kwa ushirikiano wa Klabu ya Ligi Kuu England, Sunderland, na Kampuni ya Marekani ya Nishati, Symbion.
Ndani ya Eneo hilo upo Uwanja mkubwa wa kisasa wenye Kapeti la 3G pamoja na Kiwanja cha kucheza Mechi za Timu za Wachezaji Watano dhidi ya Watano, upo Uwanja wa Mpira wa Vikapu, Mpira wa Mikono na wa Magongo.
Viwanja vyote vina Taa za kutumika Usiku na yapo ya Majengo ya Menejimenti pamoja na Vyumba vya Kubadilishia Jezi.
Akitangaza mwaliko huu kwa Vijana, Afisa Mwandamizi wa Utawala, Ismail A. Shah, amesema Timu ambazo zitahitaji kufanya mazoezi au kucheza Mechi kwa Kipindi cha kuanzia Saa 1 Usiku hadi Saa 4 Usiku, zipeleke maombi na majina kamili ya Wachezaji/Washiriki.
Kwa maelezo zaidi Waombaji wametakiwa kuwasiliana na Namba ya Simu 0714436347.
JAKAYAKIKWETE-YOUTHPARK2



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: