ITALIA YAFUZU EURO 2016, UHOLANZI, UBELGIJI NAO WAMO


MATOKEO MECHI ZA JANA KUFUZU EURO 2016
Bosnia & Herzegovina 2-0 Wales
Israel 1-2 Cyprus
Andorra 1-4 Ubelgiji
Jamhuri ya Czech 0-2 Uturuki
Croatia 3-0 Bulgaria
Iceland 2-2 Latvia
Azerbaijan 1-3 Italia
Norway 2-0 Malta
Kazakhstan 1-2 Uholanzi
Matteo Darmian akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Italia jana mjini Baku PICHA ZAIDI GONGA HAPA
ITALIA imefuzu Euro 2016 kufuatia ushindi wa ugenini wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji Azerbaijan Uwanja wa Taifa wa Baku usiku wa jana.
The Azzuri sasa inafikisha pointi 21 katika Kundi H baada ya mechi tisa kutokana na mabao ya Eder Citadin Martins dakika ya 11, Stephan El Shaarawy dakika ya 43 na Matteo Darmian dakika ya 65.
Bao la wenyeji lilifungwa na Dimitrij Nazarov dakika ya 31. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Croatia imeichapa 3-0 Bulgaria, mabao ya Ivan Perisic, Ivan Rakitic na Nikola Kalinic.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Norway imeshinda nyumbani 2-0 dhidi ya Malta, mabao ya Alexander Tettey dakika ya 19 na Alexander Soderlund dakika ya 52 Uwanja wa  
Ullevaal.
Bosnia & Herzegovina imeifunga 2-0 Wales, mabao ya Milan Djuric na Vedad Ibisevic Uwanja wa Bilino Polje katika mchezo wa Kundi B. lakini Wales imefuzu Euro 2016 kutokana na Israel kufunga 2-1 nyumbani na Cyprus katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Mchezo mwingine wa Kundi B, Ubelgiji imeshinda 4-1 ugenini dhidi ya Andorra mabao yake yakifungwa na Radja Nainggolan dakika ya 19, Kevin De Bruyne dakika ya 42, Eden Hazard kwa penalti dakika ya 56 na Laurent Depoitre dakika ya 64 Uwanja wa Comunal d'Andorra la Vella.
Bao pekee la Andorra limefungwa na Ildefonso Lima Sola kwa penalti dakika ya 51.  
Katika Kundi A, Uholanzi imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Kazakhstan Uwanja wa Astana.
Mabao ya Uholanzi yamefungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 33 na Wesley Sneijder dakika ya 50, wakati la wenyeji limefungwa na Islambek Kuat dakika ya 90+5.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Uturuki imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Jamhuri ya Czech, mabao ya Selcuk Inan kwa penalti dakika ya 62 na Hakan Calhanoglu dakika ya 79 Uwanja wa Jenerali Arena.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Iceland imelazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Latvia, mabao yake yakifungwa na Kolbeinn Sigthorsson dakika ya tano na Gylfi Sigurdsson dakika ya 27, wakati ya wageni yamefungwa na Aleksandrs Cauna dakika ya 49 na Valerijs Sabala dakika ya 68 Uwanja wa Laugardalsvollur



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: