Kwa wenzetu wa Marekani kipindi hiki ni msimu wa shindano kubwa la kusaka vipaji, American Idol…
kwa sasa bado usaili unaendelea, watu wengi wamekuwa
wakijitokeza kwa
wingi kuchukua namba zao za usaili ili kuweza kuwaonyesha majaji vipaji
walivyonavyo.
Kwa ujuzi wa watu wengi, shindano la American Idol
huwa ni maalum kwa ajili ya kusaka vipaji vipya vya wasanii wa
underground watakaoweza kutimiza ndoto zao kwenye game ya muziki Marekani… lakini inakuaje pale ambapo staa mkubwa wa muziki anaamua kushiriki shindano hilo!? Mtihani mkubwa kwa majaji sio?
Kanye West ni mtu mwenye vipaji vingi sana pia mchekeshaji mwenye vituko kiaina pia… kwenye usaili wa msimu wa mwaka huu kwenye American Idol jijini San Francisco, Kanye aliamua
kuwasuprise watu na majaji kwa ujio wake kwenye shindano hilo, sio kwa
kutoa show bali kwa kuchukua nama ya kushiriki kwenye shindano hilo
kujaribu bahati yake!
Akiwa kwenye audition yake, Kanye West aliperform wimbo wake wa ‘Gold Digger’ wimbo ulioweka tabasamu kwenye uso wa mmoja wa majaji wa shindano hilo, msanii Jennfer Lopez baada ya Kanye kumtaja kwenye wimbo huo… cha kufuraisha zaidi ni kwamba Kanye West kafanikiwa kuingia kwenye round ya pili, na kapewa tickect ya moja kwa moja kwenda Hollywood pia!
Kanye West bwana, ana vituko sana!
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment