KOMBE LA DUNIA 2018: TANZANIA YAFUNGWA NA MALAWI LAKINI YASONGA, KUIVAA ALGERIA NOV 9



TAIFASTARS-MKWASA-SHTimu ya Taifa ya Tanzania Leo imefungwa Bao 1-0 huko Uwanja wa Kamuzu Banda, Blantyre na Wenyeji Malawi katika Mechi Marudiano ya Raundi ya Kwanza ya Kanda ya Afrika ya Mchujo wa Kombe la Dunia ambazo Fainali zake zitafanyika huko Russia Mwaka 2018 lakini imesonga Raundi ya Pili kwa Jumla ya Bao 2-1 katika Mechi mbili.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Jumatano iliyopita Tanzania iliichapa Malawi 2-0 kwa Bao za Maprofeshanali Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wote hucheza huko Congo DR kwenye Klabu ya Lubumbashi TP Mazembe.

Leo, Wamalawi walicharuka na kutawala, hasa Kiungo, dhidi ya Kikosi cha Tanzania chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa na kupata Bao lao pekee la Mechi hii katika Dakika ya 41 kupitia Dave Banda.
Tanzania sasa watacheza Raundi ya Pili na Algeria ambao wanaanzia hatua hiyo ambayo Mechi zake zimepangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam Novemba 9 na Marudiano huko Algiers hapo Novemba 17.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja.
KIKOSI CHA TANZANIA:
Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’, Shomary Salum Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Kelvin Patrick Yondan, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’, Himid Mao Mkami, Said Hamisi Ndemla, Mudathir Yahya Abbas, Farid Malik Mussa, Mbwana Ally Samatta, Thomas Ulimwengu
KOMBE LA DUNIA 2018
Afrika-Raundi ya Awali- Marudiano
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Oktoba 11
Malawi v Tanzania [0-2]    
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
16:00 Ethiopia v Sao Tome And Principe [0-1]
16:00 Kenya v Mauritius [5-2]    
Jumanne Oktoba 13
14:30 Madagascar v Central African Republic [3-0]    
16:00 Burundi v Seychelles [1-0] 
17:00 Sierra Leone  v Chad [0-1]
18:00 Namibia v Gambia [1-1]    
18:00 Niger v Somalia [2-0]       
19:00 Lesotho v Comoros [0-0]
19:00 Guinea-Bissau v Liberia [1-1]      
20:00 Botswana v Eritrea [2-0]   
20:00 Swaziland v Djibouti          [6-0]
20:00 Mauritania v South Sudan [1-1]
Raundi ya Pili
**Mechi kuchezwa Novemba 9 hadi 17
Somalia/Niger v Cameroon
South Sudan/Mauritania v Tunisia
Gambia/Namibia v Guinea
Sao Tome/Ethiopia v Congo
Chad/Sierra Leone v Egypt
Comoros/Lesotho v Ghana
Djibouti/Swaziland v Nigeria
Eritrea/Botswana v Mali
Seychelles/Burundi v DR Congo
Liberia/Guinea Bissau v Ivory Coast
CAR/Madagascar v Senegal
Mauritius/Kenya v Cape Verde
Tanzania v Algeria
Sudan v Zambia
Libya v Rwanda
Morocco v Equatorial Guinea
Mozambique v Gabon
Benin v Burkina Faso
Togo v Uganda
Angola v South Africa
**Washindi kutinga hatua ya Makundi



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: