CHADEMA WAMALIZA UTATA

 

  Chama cha Chadema kimeviasa vyama vinavyounda Ukawa kuacha malumbano kuhusu majimbo na badala yake kila kimoja kisimamishe mgombea wake kwa yale yaliyo na misuguano.   Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar) na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaombea kura mgombea ubunge na madiwani wa jimbo la Handeni mjini.   Alisema wamekaa kikao na kukubaliana katika majimbo yote yaliyokuwa na malumbano kila chama hasa vya Chadema na CUF kisimamishe mgombea wagombea.   Mwalimu alisema nia ya kufanya hivyo ni kuzuia majimbo na kata zisichukuliwe na CCM. Alisema wasingefanya hivyo, wangeweza kupoteza baadhi ya kata na majimbo ambayo baadhi ya wagombea wao waliwekewa mapingamizi ambayo yalisababisha kutolewa kwenye nafasi zao.   “Tumeshakubaliana kwamba vyama vyote viwaache wagombea wake waendelee na mchakato wa kampeni na hakuna sababu za kulumbana. Sisi adui yetu ni CCM tu, hakuna uadui ndani ya upinzani au Ukawa, hivyo tangazeni uadui wa nje na siyo wa ndani,” alisisitiza Mwalimu.   Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Handeni, Jadi Bamba alisema uamuzi huo ni sahihi na wanaamini jimbo hilo haliwezi kuchukuliwa na CCM.  Akizungumzia mgawanyiko wa kura iwapo watavunja umoja huo, alisema wanawafahamu wapiga kura wao na wala CCM haina ubavu wa kushinda.   Hata hivyo, mwanachama wa Chadema wilayani Handeni, Kisaga Salehe alisema uamuzi huo si sahihi na utadhoofisha ushindani katika majimbo na kutoa mwanya kwa vyama vingine kama CCM kushinda kirahisi
Chama cha Chadema kimeviasa vyama vinavyounda Ukawa kuacha malumbano kuhusu majimbo na badala yake kila kimoja kisimamishe mgombea wake kwa yale yaliyo na misuguano. 

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar) na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaombea kura mgombea ubunge na madiwani wa jimbo la Handeni mjini. 

Alisema wamekaa kikao na kukubaliana katika majimbo yote yaliyokuwa na malumbano kila chama hasa vya Chadema na CUF kisimamishe mgombea wagombea. 

Mwalimu alisema nia ya kufanya hivyo ni kuzuia majimbo na kata zisichukuliwe na CCM. Alisema wasingefanya hivyo, wangeweza kupoteza baadhi ya kata na majimbo ambayo baadhi ya wagombea wao waliwekewa mapingamizi ambayo yalisababisha kutolewa kwenye nafasi zao. 

“Tumeshakubaliana kwamba vyama vyote viwaache wagombea wake waendelee na mchakato wa kampeni na hakuna sababu za kulumbana. Sisi adui yetu ni CCM tu, hakuna uadui ndani ya upinzani au Ukawa, hivyo tangazeni uadui wa nje na siyo wa ndani,” alisisitiza Mwalimu. 

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Handeni, Jadi Bamba alisema uamuzi huo ni sahihi na wanaamini jimbo hilo haliwezi kuchukuliwa na CCM.

Akizungumzia mgawanyiko wa kura iwapo watavunja umoja huo, alisema wanawafahamu wapiga kura wao na wala CCM haina ubavu wa kushinda. 

Hata hivyo, mwanachama wa Chadema wilayani Handeni, Kisaga Salehe alisema uamuzi huo si sahihi na utadhoofisha ushindani katika majimbo na kutoa mwanya kwa vyama vingine kama CCM kushinda kirahisi. 
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/10/chadema-yavunja-makubaliano-ukawa.html#sthash.p4bcLD6N.dpuf


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: