Waliokufa mgodini Kahama ndio basi tena

Waliokufa mgodini Kahama ndio basi tena?

Jitihada za kuwafukua wachimbaji saba waliokufa katika mgodi wa Nyangalata wilayani Kahama zimegonga mwamba baada ya Serikali kudai shughuli ya kuwatoa itachukua miezi miwili. Hali hiyo ilielezwa juzi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipotembelea eneo hilo.

 Alisema tayari wataalamu kutoka Kampuni ya Acacia Bulyanhulu wamechunguza na kubaini wachimbaji hao wamefukiwa umbali wa mita 120 kutoka usawa wa ardhi. Kitwanga anayeshughulikia madini katika wizara hiyo alisema kuwatoa watu hao ni kazi ngumu inayohitaji mitambo mikubwa yenye uwezo wa kufukua eneo lote la mgodi ili kuwafikia. 

Alisema kutokana na changamoto iliyopo, kazi hiyo inahitaji muda mrefu na wataalamu zaidi. Hata hivyo, Kitwanga amewataka wachimbaji na wananchi wenye mbinu za uokoaji watoe ushauri wenye kuweza kutumika kuwatoa marehemu hao ambao hadi sasa bado juhudi za kuwatambua zinaendelea. 

Wachimbaji hao wiki iliyopita walifukiwa na kifusi wakiwa kazini wakichimba dhahabu kwenye mashimo hayo. 

Katika tukio hilo wachimbaji kumi na moja waliokolewa siku hiyo na mmoja kutolewa akiwa amefariki dunia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema katika wachimbaji saba walioshindwa kuokolewa, awali walikuwa wakiwasiliana na wenzao wa nje kwa simu ili wasaidiwe kabla ya mauti kuwakumba. 

Kamanda Kamugisha alisema juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao ziligonga mwamba kutokana na umbali uliokuwapo kutoka juu ya ardhi na kule walikokuwa wamefukiwa na kifusi cha udongo.
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/10/waliokufa-mgodini-kahama-ndio-basi-tena.html#sthash.wtijNgDg.dpuf

CHADEMA "yavunja" makubaliano UKAWA

Chama cha Chadema kimeviasa vyama vinavyounda Ukawa kuacha malumbano kuhusu majimbo na badala yake kila kimoja kisimamishe mgombea wake kwa yale yaliyo na misuguano. 

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar) na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaombea kura mgombea ubunge na madiwani wa jimbo la Handeni mjini. 

Alisema wamekaa kikao na kukubaliana katika majimbo yote yaliyokuwa na malumbano kila chama hasa vya Chadema na CUF kisimamishe mgombea wagombea. 

Mwalimu alisema nia ya kufanya hivyo ni kuzuia majimbo na kata zisichukuliwe na CCM. Alisema wasingefanya hivyo, wangeweza kupoteza baadhi ya kata na majimbo ambayo baadhi ya wagombea wao waliwekewa mapingamizi ambayo yalisababisha kutolewa kwenye nafasi zao. 

“Tumeshakubaliana kwamba vyama vyote viwaache wagombea wake waendelee na mchakato wa kampeni na hakuna sababu za kulumbana. Sisi adui yetu ni CCM tu, hakuna uadui ndani ya upinzani au Ukawa, hivyo tangazeni uadui wa nje na siyo wa ndani,” alisisitiza Mwalimu. 

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Handeni, Jadi Bamba alisema uamuzi huo ni sahihi na wanaamini jimbo hilo haliwezi kuchukuliwa na CCM.

Akizungumzia mgawanyiko wa kura iwapo watavunja umoja huo, alisema wanawafahamu wapiga kura wao na wala CCM haina ubavu wa kushinda. 

Hata hivyo, mwanachama wa Chadema wilayani Handeni, Kisaga Salehe alisema uamuzi huo si sahihi na utadhoofisha ushindani katika majimbo na kutoa mwanya kwa vyama vingine kama CCM kushinda kirahisi
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/10/chadema-yavunja-makubaliano-ukawa.html#sthash.na6tG3w4.dpuf

Waliokufa mgodini Kahama ndio basi tena? By Edwin Moshi at Monday, October 12, 2015 Jitihada za kuwafukua wachimbaji saba waliokufa katika mgodi wa Nyangalata wilayani Kahama zimegonga mwamba baada ya Serikali kudai shughuli ya kuwatoa itachukua miezi miwili. Hali hiyo ilielezwa juzi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipotembelea eneo hilo.   Alisema tayari wataalamu kutoka Kampuni ya Acacia Bulyanhulu wamechunguza na kubaini wachimbaji hao wamefukiwa umbali wa mita 120 kutoka usawa wa ardhi. Kitwanga anayeshughulikia madini katika wizara hiyo alisema kuwatoa watu hao ni kazi ngumu inayohitaji mitambo mikubwa yenye uwezo wa kufukua eneo lote la mgodi ili kuwafikia.   Alisema kutokana na changamoto iliyopo, kazi hiyo inahitaji muda mrefu na wataalamu zaidi. Hata hivyo, Kitwanga amewataka wachimbaji na wananchi wenye mbinu za uokoaji watoe ushauri wenye kuweza kutumika kuwatoa marehemu hao ambao hadi sasa bado juhudi za kuwatambua zinaendelea.   Wachimbaji hao wiki iliyopita walifukiwa na kifusi wakiwa kazini wakichimba dhahabu kwenye mashimo hayo.   Katika tukio hilo wachimbaji kumi na moja waliokolewa siku hiyo na mmoja kutolewa akiwa amefariki dunia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema katika wachimbaji saba walioshindwa kuokolewa, awali walikuwa wakiwasiliana na wenzao wa nje kwa simu ili wasaidiwe kabla ya mauti kuwakumba.   Kamanda Kamugisha alisema juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao ziligonga mwamba kutokana na umbali uliokuwapo kutoka juu ya ardhi na kule walikokuwa wamefukiwa na kifusi cha udongo

Waliokufa mgodini Kahama ndio basi tena?

Jitihada za kuwafukua wachimbaji saba waliokufa katika mgodi wa Nyangalata wilayani Kahama zimegonga mwamba baada ya Serikali kudai shughuli ya kuwatoa itachukua miezi miwili. Hali hiyo ilielezwa juzi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipotembelea eneo hilo.

 Alisema tayari wataalamu kutoka Kampuni ya Acacia Bulyanhulu wamechunguza na kubaini wachimbaji hao wamefukiwa umbali wa mita 120 kutoka usawa wa ardhi. Kitwanga anayeshughulikia madini katika wizara hiyo alisema kuwatoa watu hao ni kazi ngumu inayohitaji mitambo mikubwa yenye uwezo wa kufukua eneo lote la mgodi ili kuwafikia. 

Alisema kutokana na changamoto iliyopo, kazi hiyo inahitaji muda mrefu na wataalamu zaidi. Hata hivyo, Kitwanga amewataka wachimbaji na wananchi wenye mbinu za uokoaji watoe ushauri wenye kuweza kutumika kuwatoa marehemu hao ambao hadi sasa bado juhudi za kuwatambua zinaendelea. 

Wachimbaji hao wiki iliyopita walifukiwa na kifusi wakiwa kazini wakichimba dhahabu kwenye mashimo hayo. 

Katika tukio hilo wachimbaji kumi na moja waliokolewa siku hiyo na mmoja kutolewa akiwa amefariki dunia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema katika wachimbaji saba walioshindwa kuokolewa, awali walikuwa wakiwasiliana na wenzao wa nje kwa simu ili wasaidiwe kabla ya mauti kuwakumba. 

Kamanda Kamugisha alisema juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao ziligonga mwamba kutokana na umbali uliokuwapo kutoka juu ya ardhi na kule walikokuwa wamefukiwa na kifusi cha udongo.
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/10/waliokufa-mgodini-kahama-ndio-basi-tena.html#sthash.wtijNgDg.dpuf

Waliokufa mgodini Kahama ndio basi tena?

Jitihada za kuwafukua wachimbaji saba waliokufa katika mgodi wa Nyangalata wilayani Kahama zimegonga mwamba baada ya Serikali kudai shughuli ya kuwatoa itachukua miezi miwili. Hali hiyo ilielezwa juzi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipotembelea eneo hilo.

 Alisema tayari wataalamu kutoka Kampuni ya Acacia Bulyanhulu wamechunguza na kubaini wachimbaji hao wamefukiwa umbali wa mita 120 kutoka usawa wa ardhi. Kitwanga anayeshughulikia madini katika wizara hiyo alisema kuwatoa watu hao ni kazi ngumu inayohitaji mitambo mikubwa yenye uwezo wa kufukua eneo lote la mgodi ili kuwafikia. 

Alisema kutokana na changamoto iliyopo, kazi hiyo inahitaji muda mrefu na wataalamu zaidi. Hata hivyo, Kitwanga amewataka wachimbaji na wananchi wenye mbinu za uokoaji watoe ushauri wenye kuweza kutumika kuwatoa marehemu hao ambao hadi sasa bado juhudi za kuwatambua zinaendelea. 

Wachimbaji hao wiki iliyopita walifukiwa na kifusi wakiwa kazini wakichimba dhahabu kwenye mashimo hayo. 

Katika tukio hilo wachimbaji kumi na moja waliokolewa siku hiyo na mmoja kutolewa akiwa amefariki dunia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema katika wachimbaji saba walioshindwa kuokolewa, awali walikuwa wakiwasiliana na wenzao wa nje kwa simu ili wasaidiwe kabla ya mauti kuwakumba. 

Kamanda Kamugisha alisema juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao ziligonga mwamba kutokana na umbali uliokuwapo kutoka juu ya ardhi na kule walikokuwa wamefukiwa na kifusi cha udongo.
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/10/waliokufa-mgodini-kahama-ndio-basi-tena.html#sthash.wtijNgDg.dpuf

Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: