WANAOKAMATA Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu England Manchester United wapo kwao Old Trafford Jumamosi Jioni kucheza na Timu ya mkiani Sunderland.
Timu zote hizi mbili zinatoka kwenye Mechi za kati ya Wiki za Kombe la Ligi, Capital One Cup, ambazo Man United waliitwanga Ipswich Town 3-0 na Sunderland kufungwa Ugenini Uwanjani Etihad Jijini Manchester Bao 4-1 na Man City.
Hicho kilikuwa kipigo cha 3 mfululizo kwa Sunderland ambao pia walichapwa 2-0 Ugenini na Bournemouth na 1-0 na Tottenham.
Mara ya mwisho kwa Man United kucheza na Sunderland Uwanjani Old Trafford ilikuwa Februari Mwaka huu na Man United kushinda 2-0.
Hali za Wachezaji
Baada ya kuwachezesha tangu mwanzo kwa mara ya kwanza Msimu huu Antonio Valencia na Andreas Pereira, Louis van Gaal huenda akawarudisha Kikosini Matteo Darmian na Memphis Depay huku Phil Jones, ambae alikuwa majeruhi na kucheza Dakika 21 alipoingizwa toka Benchi kwenye Mechi na Ipswich, huenda akatoa mchango wakati fulani wa Mechi hii na Sunderland.
Nae Bosi wa Sunderland Dick Advocaat, ambae anatoka Holland kama Louis van Gaal, atamkosa Adam Matthews, ambae ameumia, lakini anaweza kuwatumia Costel Pantilimon, Billy Jones, Jordi Gomez na Jermain Defoe ambao hawakucheza Mechi na Man City.
Pia, Younes Kaboul, ambae amemaliza kifungo, na Beki wa zamani wa Man United, John O'Shea, huenda wakacheza.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Manchester United: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Darmian, Carrick, Schneiderlin, Mata, Memphis, Rooney, Martial
Sunderland: Pantilimon; Yedlin, Kaboul, Coates, van Aanholt; M'Vila, Cattermole; Toivonen, Lens, Larsson; Borini
REFA: Mike Jones
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Ligi Kuu England:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 2
1445 Tottenham v Man City
1700 Leicester v Arsenal
1700 Liverpool v Aston Villa
1700 Man United v Sunderland
1700 Southampton v Swansea
1700 Stoke v Bournemouth
1700 West Ham v Norwich
1930 Newcastle v Chelsea
Jumapili Septemba 27
1800 Watford v Crystal Palace
Jumatatu Septemba 28
2200 West Brom v Everton
MSIMAMO:
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment