BECKHAM AKUBALIANA NA SIR ALEX FERGUSON KUWA YEYE ‘SI KIWANGO CHA DUNIA!’

 SIRALEX-BECKHAMMCHEZAJI wa zamani wa Manchester United David Beckham amekubaliana na tathmini ya Sir Alex Ferguson kwamba yeye hakuwa na ‘kiwango cha Dunia’ katika uchezaji Soka.
Katika chapisho jipya la Kitabu cha maisha ya Sir Alex Ferguson kuna madai kuwa katika himaya yake kama Meneja wa Manchester United alisimamia Wachezaji Wanne tu wenye kustahili hadhi ya kuwa Wachezaji wa Kiwango cha Dunia.
David Beckhama, ambae pia alikuwa Kepteni wa Timu ya Taifa ya England, hayumo kwenye Listi hiyo ya Wachezaji hao Wanne ambao ni Cristiano Ronaldo, Ryan Giggs, Paul Scholes na Eric Cantona.

Akihojiwa na BBC, Shirika la Habari la Uingereza, kama kutokuwepo kwenye Listi hiyo ni ‘tusi’ kwake, Beckham alijibu: “Hapana kabisa.”
Alieleza: “Nimecheza chini ya Meneja Bora katika Historia yote kwa muda niliocheza, nilibahatika kucheza na Wachezaji niliocheza nao na kupata mafanikio makubwa kwa Klabu niliyoipenda na bado naipenda.”
Aliongeza: “Nakubaliana na Meneja. Wapo kwa hakika Wachezaji unaoweza kuwaita wa kiwango cha Dunia na nashukuru nilicheza na wengi wao.”
Beckham alisema zaidi: “Nasikia fahari kama Mchezaji wa Manchester United kwamba tulifanikiwa na nasikia fahari kama Mchezaji wa Manchester United kwamba Wachezaji Bora walikuja Timu yetu.”


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment