SERIE A-JUMAMOSI VITA YA TIMU ZA MASHAKANI NAPOLI NA JUVENTUS

SERIEA-JUVEJUMAMOSI Stadio San Paolo itashuhudia Mechi kali ya Timu kongwe huko Italy, Napoli na Juventus, ambazo Msimu huu zipo mashakani mno.SERIEA-TEBO-SEP25 Juventus, Mabingwa Watetezi wa Italy kwa Misimu Minne mfululizo, Msimu huu wameanza utetezi wao kwa mguu mbaya baada ya kuambua
Pointi 5 tu katika Mechi 5 walizocheza na wapo Nafasi ya 13 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Inter Milan.
Lakini pia wapinzani wao wa Jumamosi, Napoli, wako hali kama yao na wapo Pointi 1 tu juu yao.
Licha ya Timu hizi kusuasua lakini Mechi zao zote kawaida huzaa si chini ya Goli 3 na Napoli hutegemea Zaidi nguvu ya Kiungo wao Lorenzo Insigne akiungana na Allan pamoja na Marek Hamsik huku Gonzalo Higuain akiongoza mashambulizi.
Juve ndio wapo mashakani hasa wakikabiliwa na majeruhi kibao wakiwemo Alvaro Morata, Mario Mandzukic na Stephan Lichtsteiner na majeruhi wao wa muda mrefu Claudio Marchisio, Kwadwo Asamoah na Sami Khedira
Kwenye Mechi kama hii Msimu uliopita Napoli, wakiwa kwao, walitandikwa 3-1 na Juventus.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Napoli: Reina; Hysaj, Albiol, Koulibaly, Ghoulam; Allan, Jorginho, Hamsik; Callejon, Higuain, Insigne
Juventus: Buffon; Caceres, Barzagli, Chiellini, Evra; Sturaro, Hernanes, Pogba; Cuadrado, Morata, Dybala
SERIE A
RATIBA
Jumamosi Septemba 26
1900 AS Roma v Carpi
2145 SSC Napoli v Juventus FC
Jumapili Septemba 27
1330 Genoa CFC v AC Milan
1600 Bologna FC v Udinese Calcio
1600 Torino FC v U.S. Citta di Palermo
1600 Hellas Verona FC v SS Lazio
1600 US Sassuolo Calcio v AC Chievo Verona
2145 Inter Milan v ACF Fiorentina
Jumatatu Septemba 28
2000 Frosinone Calcio v Empoli
2200 Atalanta v UC Sampdoria

Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment