TANLEY KOLIMBA ASEMA ALIKUWA NA UWEZO MDOGO SANA WA KUWASAIDIA WANALUDEWA

 

       Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa njombe Ndg Stanley Kolimba.

 


              Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi ccm tawi la kilimahewa


                          Viongozi wa ccm tawi la KIlimahewa Ludewa,


    Watatu kutoka kulia ni mgombea kiti cha udiwani kata ya Ludewa Bi, Monica Mchilo,
 

       Katibu wa mgombea kiti cha Ubunge katika jimbo la Ludewa Mh, Deo Filikunjombe bw, STanley Gowele akizungumza na wanachama wa tawi la kilimahewa wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe,


                     Stanley Gowele katibu wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa Mh, Deo Filikunjombe,

Na www.maikoluoga.blogsport.com     Kolimba ameyasema hayo mapema hii leo september 22 mwaka huu katika viwanja vya mkutano Kilimahewa alipokuwa akiwanadi wagombea wa Udiwani katika kaya Ludewa mjini na Mgombea ubunge jimbo la Ludewa Mh, Deo filikunjombe ambaye hakuwepo uwanjanihapo kutokana na majukumu ya Chama cha mapinduzi ccm na kuwakilishwa na katibu wake Mh, Stanley Gowele.

Alisema kuwa Enzi za utawala wake kama Mbunge hajawahi kusomesha wanafunzi kwa nguvu zake binafsi kama alivyofanya Filikunjombe hivyo anaamini kuwa Filikunjombe ni mtu wawatu na anaaamini kuwa mgombea huyo anakipaji cha pekee kwa manufaa ya watu wa Ludewa.


Kolimba ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ludewa ambae aliwataka wanachama wa ccm wilaya ya LUdewa kumchagua Dk. John Pombe Magufuli kuwa Raisi wao na Mh, Deo Filikunjombe Haule kuwa MBUNGE wAO Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kwa lengo la kujiinua kiuchumi katika maisha yao ya baadae.

Stanley Gowele ni katibu wa Mgombea ubunge kupitia ccm Mh, DEO Filikunjombe ambaye alisema kuwa wanachama wa ccm wanatakiwa kuchagua viongozi wa ccm kwakuwa ndio wanaijua serikali ya chama chao hivyo itakuwa rahisi kuendeleza maendeleo waliyoyaacha kwa kipindi hiki kinachopita.

Aliongeza kuwa Deo Filikunjombe analengo la kuwainua wananchi wa Ludewa kiuchumi kwa kuanzisha Elimu ya ujasiliamali kwa kila mwananchi wa Ludewa mara tu atakapo chaguliwa ili kla mmoja aweze kujitegemea katika maisha yake ya kila siku.


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment